Washindi wa Mwanaspoti wafurahia mchongo

Muktasari:

DROO ya pili ya Promosheni shinda mchongo wa Mwanaspoti imetoa washindi sita waliojishindia pesa taslimu shilingi laki moja kila mmoja na mmoja akijishindia simu ya mkononi.

DROO ya pili ya Shinda Mchongo wa Mwanaspoti imetoa washindi sita jana Ijumaa kuna walioshinda pesa taslimu Sh 100,000 na simu ya kisasa ya mkononi (smartphone).
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, washindi hao wlaielezea hisia zao juu ya ushindi huo licha ya kwamba ushindani ulikuwa mkubwa kutokana na wasomaji wengi kushindania zawadi hizo.
Dinah Edward kutoka Kigogo jijini Dar es Salaam ni kati ya washindi walioshinda pesa taslimu alisema anajisikia furaha kubwa na kuwashauri Watanzania kuendelea kusoma Mwanaspoti pamoja na kucheza mchezo huo.
“Unajua sio lazima uangalie mpira kwenye televisheni, mimi nikisoma Mwanaspoti napata habari za ndani mpaka nje kwahiyo nawashauri wenzangu nao wasome,” alisema.
Naye Hamza Juma (Tandika) alisema anajisikia furaha kuwa mshindi wa Mwanaspoti kwani amekuwa ni mtu anayefuatilia habari zinazoandikwa na gazeti la Mwanaspoti mara kwa mara.
“Mimi nimekuwa mtu wa kulisoma gazeti hili la Mwanaspoti na Mwananchi pia, kwahiyo kuwa mshindi ni jambo zuri kwangu napenda kuwaambia wengine nao wasome magazeti haya,” alisema.
Wakati huo huo, Shaban Bakly mshindi kutoka Mkuranga, alisema ni jambo la kheri kuibuka mshindi katika mchezo huu wa bahati nasibu na ameahidi kuendelea kucheza.
Washindi wa droo hiyo ya Mwanaspoti waliojipatia Sh 100,000, Joseph Mwasumbi (Mbeya), Hamza Juma(Tandika), Shaban Bakly (Mkuranga), Dinah Edward (Kigogo Kati), Pharles Mgongo (Kibaha) na Abyud Kipanda (Mbeya) aliyejishindia simu ya kisasa (Smartphone).