Usajili Ulaya wafungwa kibabe

Muktasari:

Majogoo wa jiji Liverpool watacheza leo majira ya saa 4;00 usiku  dhidi ya Norwich City kwenye uwanja wao wa  Anfield mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu England msimu huu wa 2019/20.

MAJIRA  haya ya kiangazi imetumika  jumla ya Pauni 1.41  bilioni kwa  usajili uliofanywa na timu zote za Ligi Kuu nchini  England , ambazo zilikuwa  zikiinyemelea rekodi  ya 2017 kwa mujibu wa Deloitte ambapo ilitumika Pauni 1.43  bilion.
Wale vigogo wa Ligi hiyo peke yao kwenye kiasi hicho cha fedha, wametumia Pauni 170 millioni katika madili 17 siku ya mwisho ya usajili hicho ni kiasi kidogo cha fedha ukilinganisha na awamu zilizopita za majira ya kiangazi.
Everton ilimnasa dakika za mwisho, Alex Iwobi  kutoka  Arsenal kwa  Pauni  34 millioni, pia katika dili la  Romelu Lukaku kujiunga na Inter Milan ya Italia ilishuhudiwa mashetani wekundu wa Old Trafford wakipata hasara ya Pauni 1 million kutokana na kumuuza  kwao kwa Pauni  74 millioni.
Arsenal awamu hii, wameonekana kutotaka mchezo kabisa majira haya kwa kwa kutumia  Pauni 155millioni.Siku ya mwisho ya usajili, walimchukua  beki wa kushoto wa Celtic, Kieran Tierney kwa Pauni 25 millioni   na  walitoa  Pauni 8millioni kwa  Chelsea ili wamnase beki wa kati, David Luiz.
Tottenham  walimsajili   kiungo  kutoka  Real Betis,  Giovani lo Celso kwa mkopo  na  pia waliipata saini ya  Ryan Sessegnon  kwa Pauni 25millioni  kutoka  Fulham huku dili la kuchukua Paulo Dybala wa Juventus  likigonga mwamba.
Watford wao waliweka rekodi   kwa kutumia  Pauni  25millioni , kumsajili winga kutoka  Rennes ya  Ufaransa, Ismaila Sarr. Leicester  waliinasa saini ya kiungo mshambuliaji wa  Sampdoria, Dennis Praet kwa  Paundi  18millioni.
Wafuatao ni wachezaji wapya waliosajiliwa na  vigogo wa Ligi hiyo, Arsena, Nicolas Pepe (Lille, £72m) , William Saliba (Saint Etienne, £27m), Kieran Tierney (Celtic, £25m), David Luiz (Chelsea, £7m), Gabriel Martinelli (Ituano, £6m), Dani Ceballos (Real Madrid, £15m - mkopo).
Chelsea Mateo Kovacic (Real Madrid, £40m). Manchester City , Rodri (Atletico Madrid, £63m), Joao Cancelo (Juventus, £60m), Angelino (PSV, £5.3m), Morgan Rogers (West Bromwich Albion, £4m) na Scott Carson (Derby County, mkopo).
Manchester United, Harry Maguire (Leicester City £80m), Aaron Wan-Bissaka (Crystal Palace, £50m) na Daniel James (Swansea City, £17m).
Tottenham, Tanguy Ndombele (Lyon, £65m),Ryan Sessegnon (Fulham, £25m), Jack Clarke (Leeds United, £11.5m), Kion Etete (Notts County, imefichwa ) na Giovani lo Celso (Real Betis,mkopo).
Liverpool, Sepp van den Berg (PEC Zwolle, £4.4m), Adrian (West Ham United,bure)na Harvey Elliott (Fulham).