Simba yainyofoa Yanga kileleni

Muktasari:

  • Mechi hiyo ilikuwa na ushindani mkali kutokana na ubora wa vikosi vya timu zote ambapo bao la Simba lilipatikana katika dakika za nyongeza za mwamuzi baada ya 90 kumalizika kisha kuongezwa dakika 3.

Kikosi cha Simba kimetoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo Jumapili.

Mechi hiyo ilikuwa na ushindani mkali kutokana na ubora wa vikosi vya timu zote ambapo bao la Simba lilipatikana katika dakika za nyongeza za mwamuzi baada ya 90 kumalizika kisha kuongezwa dakika 3.

Ushindi huo unawafanya Simba kupanda kileleni wakiwa na pointi 12 ambazo ni sawa na Yanga lakini wakitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa.

Bao la Simba liliwekwa wavuni na Emmanuel Okwi huku Mtibwa wakianza kufunga bao lao katika kipindi cha kwanza lililotandikwa na Stamili Mbonde.