Ruvu Shooting wapo tayari kukipiga

Muktasari:

Ndio raha ya kuwa na wachezaji wazawa hawa wa kigeni hawana ishu hawa sisi tunaamini sana wazawa

RUVU Shooting ya Pwani imesema inajivunia kuwa na wachezaji wazawa watupu wenye uwezo mkubwa kuzidi wa kigeni wanaocheza timu nyingine nchini.
Mkuu wa Idara ya Habari ya Klabu hiyo, Masau Bwire kuwa, hawana shaka yoyote mpaka sasa endapo Serikali itarejesha michezo baada ya siku 30 walizozuia kuwepo na mikusnayiko.
Amesema kuwa wachezaji wao wote wapo nchini hawana hilo pekee linawafanya wasiwe na shaka wala wasiwasi hata wakitangaziwa ligi kuendelea kesho.
"Ruvushooting sio waumini wa kuamini wachezaji wa nje kuliko wazawa, wazawa wanaweza sana tena uwezo wao uko juu tofauti na wa kigeni na ndio maana tunajivunia,"amesema.
Masau amesema timu yenye wachezaji wa nje kwasasa zinahaha kwani wakirejea nyota wao wanatakiwa kukaa karantini siku 14 wao hawana kitu kama hicho.