Neymar amwaga pesa ya corona

Muktasari:

Neymar ametoa mchango huo bila ya kutaka kufahamika, lakini televisheni moja ya huko Brazil kupitia kipindi chake cha Fofocalizando kimefichua jambo hilo.
Dunia kwa sasa imekua ikihamasisha mastaa mbalimbali kutoa pesa za kuchangia pambano ya janga hilo.

PARIS, HISPANIA . SUPASTAA wa Paris-Saint Germain, Neymar ametoa mkwanja mrefu kuchangia pambano dhidi ya janga la virusi vya corona.
Fowadi huyo wa Brzil kwa sili amechagia Pauni 769,000 huko UNICEF na kuungana na watu wengine maarufu katika kuchangia pesa kupambana na janga la corona.
Pesa hizo zitatumika kwenye kununua vifaa tuzo kwa ajili ya maradhi hayo na kusaidia yale maeneo yaliyoathirika zaidi.
Neymar ametoa mchango huo bila ya kutaka kufahamika, lakini televisheni moja ya huko Brazil kupitia kipindi chake cha Fofocalizando kimefichua jambo hilo.
Dunia kwa sasa imekua ikihamasisha mastaa mbalimbali kutoa pesa za kuchangia pambano ya janga hilo.
Mastaa mbalimbali akiwamo mkali wa tenisi, Novak Djokovic amechangia Pauni 877,000 kununulia vifaa tiba huko kwao Serbia.
Kumekuwa na wito wa wanasoka mbalimbali kuchangia, huku staa wa zamani wa Carlos Tevez akitaka kamba wanasoka wasilipwe mishahara kwa mwaka mzima na pesa hizo zielekezwe kwenye mapambano dhidi ya janga la corona.
Lionel Messi aliripotiwa kuchangia Euro 1 milioni kwenye vita hiyo, sambamba na kocha Pep Guardiola, aliyechangia kiwango kama hicho cha pesa kwa ajili ya mapambano ya corona huko Hispania, huku Cristiano Ronaldo akikubali kukatwa kiasi cha Pauni 3.5 milioni kwenye mshahara wake huko Juventus ili pesa hiyo itumike kwenye mambo hayo ya kuhakikisha corona inashindwa.