Molinga hashikiki huko, Yanga wanacheka tu

Muktasari:

Hadi sasa nyota huyo ndiye anaongoza kwa ufungaji mabao akiwa ametupia matatu katika mechi za kirafiki,ambapo awali wakikipiga na Pamba alitupia moja na sasa mawili.

Mwanza. Ukisikia kazi imeanza ndio hivyo.Kwa sasa Straika wa Yanga David Molinga hashikiki na katika kudhihirisha hilo,leo amefanya kweli katika dakika 45 za kwanza akitupia mabao mawili akitumia kichwa chake.

Katika mchezo huo,Nyota huyo raia wa DR Congo ameipeleka timu hiyo mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 2-0 dhidi ya Toto Africans.

Katika mchezo huo, Yanga walionekana kuwazidi wapinzani,huku wakishambulia mwanzo mwisho na kama umakini ungekuwapo zaidi,wangeweza kwenda mapumziko kwa idadi kubwa ya mabao.

Hata hivyo nao Toto walijaribu kuonyesha makeke yao,lakini mashambulizi yao hayakuwa na madhara langoni mwa Yanga.

Molinga alianza kutikisa nyavu dakika ya 36 akiunganisha pasi iliyokuwa inaelekea langoni ikitoka kwa Sadney Khoetage na dakika ya 40 akapachika la pili akiunganisha kwa kichwa shuti la Ally Mtoni.