Mo Ibrahim na wenzake watajwa Namungo

Thursday January 30 2020

 Mo Ibrahim na wenzake watajwa Namungo-Kocha wa Namungo FC- Mrundi Hitimana Thiery-Simba SC-Mbeya City vs JKT Tanzania

 

By Doris Maliyaga

Dar es Salaam.Kocha wa Namungo FC, Mrundi Hitimana Thiery amesema kufungwa kwao na Simba SC hakukusabishwa ni kukosekana kwa nyota wake watatu.

Katika mchezo huo ambao Namungo ilikubali kipigo cha mabao 3-2 kutoka kwa Simba iliwakosa nyota wake watatu Mohammed Ibrahim 'Mo', Mpinga Masabo na nahodha Mgunya Hamis.

"Kukosekana kwao siyo sababu ya sisi kufungwa, lakini kutokuwepo kwao ni pengo kwetu. Wale ni wachezaji wazoefu wana mchango wao,"alisema Hitimana.

Alisema, katika mchezo huo uliona upande wa uzoefu katika timu mbele ni kama alikuwepo Kikoti (Lucas) peke yake kama wao wangekuwepo wangesaidiana.

Akizungumzia kwa nini waligoma kuingia vyumbani, Hitimana alisema tatizo lilikuwa hewa.

"Hakukuwa na hewa nzuri vyumbani na harufu isiyoeleweka, nafikiri si dhambi kukaa nje ya vyumba," alisisitiza Hitimana.

Advertisement

Namungo imeondoka Dar es Salaam leo Alhamisi kwenda kujiandaa na mchezo mwingine wa ligi dhidi ya Mbao FC.

Advertisement