Michuano ya Sportpesa yamwibua Stam

Muktasari:

KOCHA wa Mbao FC, Amri Said 'Jaap Stam' ameanza mapema kulichangamkia dirisha dogo la usajili kwa kuimarisha kikosi chake ambacho kinashiriki Ligi Kuu Bara kwa msimu wa tatu kwa kunasa nyota wawili.

MBAO FC imesema itatumia vyema fursa ya kushiriki michuano ya Sportpesa kuhakikisha inaonyesha ushindani mkali na kutwaa ubingwa wa mashindano hayo.

Mbao itashirikishi michuano hiyo kama timu mwalikwa katika ya timu nane kutoka Tanzania na Kenya.

Kocha wa Mkuu wa timu hiyo, Amri Said ‘Stam’ alisema hiyo ni fursa muhimu kwao kuhakikisha wanaitumia vyema kujitangaza kimataifa kupitia.

Aliongeza mechi za Ligi Kuu haziwezi kumharibia mipango kwani ana kikosi kipana kinachoweza kushiriki michuano yote kwa wakati mmoja na kuonyesha soka safi.

“Ni fursa kubwa kwetu kuonyesha ubora wetu, sidhani kama Ligi Kuu itaathiri chochote kwa sababu kikosi changu kina vijana wenye uwezo kwenye soka, lazima tutwae ubingwa na kujitangaza kimataiafa,” alisema Stam.

Stam alisema michuano hiyo, Mbao inawakilisha Mikoa ya Kanda ya Ziwa hivyo lazima ifanye kweli ili kuweka rekodi mpya kwa mara ya kwanza katika mashindano hayo.

Alisisitiza wadau na mashabiki wa soka wasubiri kuona burudani kwani Mbao ni timu yenye ushindani bila kujali aina ya ligi watakayoshiriki.

“Mbao inawakilisha Mwanza lakini hata mikoa ya Kanda ya Ziwa wanatutegemea, tutafanya vyema ili kuwapa raha wadau wetu kila wanapotufatilia, kwahiyo lazima tupambane na kuwawakilisha vilivyo, hivyo wadau na mashabiki tunaomba watusapoti kwani tumejipanga kuwapa furaha,” alisema Kocha huyo.