Jaguar afuata penzi la Diva Bongo

Tuesday July 30 2019

 

MWANAMUZIKI wa Bongo, Lulu Diva kafichua kwamba yupo kwenye mahusiano ya kimapenzi na mbunge wa Starehe, Jaguar.
Akifunguka na gazeti moja la Kibongo hivi majuzi, Diva alifichua kwamba uhusiano wao umedumu kwa miezi minne sasa.
“Mapenzi yetu wala sio ya ghafla kama wanavyodhani watu, Tulianza kama miezi minne nyuma na sasa tumeamua kuweka wazi,” Lulu Diva alifunguka.
Kauli hiyo imepelekea kusadikisha safari za  mara kwa mara zake Jaguar kwenda Tanzania.
Miezi miwili iliyopita Jaguar akiwa Tanzania alifanya mahojiano na Clouds FM na kusema alikuwa kule kwa ajili ya likizo ndogo tu.
Jaguar anafahamika sana kuwa msiri sana kwenye maisha yake ya kimahusiano na ingawaje Lulu kafunguka hasa baada ya picha yao wakila bata kuibuka mitandaoni, yeye ameamua kusalia kimya.

Advertisement