Harmonize afichua msoto mkali WCB

Friday February 1 2019

 

By RHOBI CHACHA

ACHANA na ishu ya kutemwa na meneja wake, Joel Vincent ‘Mr Puaz’ staa wa Bongo Flava kutoka lebo ya WCB, Harmonize amefunguka msoto uliopo ndani ya kundi hilo kwa sasa.

Harmonize maarufu Konde Boy, amesema ndani ya lebo hiyo kila msanii kisu kutokana na uwezo mkubwa wa kuandika mashairi na kufanya shoo hivyo, kuwabamba mashabiki kila kona.

Hata hivyo, amesema ugumu zaidi ni pale unapofanya kazi na wasanii wenye uwezo kwa sababu kila mmoja anataka kutoa ngoma kali ili kumfunika mwekzake.

“Hapa WCB kuna vichwa hatari sana vya muziki, ndio sababu ugumu unakuja ni pale unapofanya kazi na wasanii ambao wana uwezo, ushindani katika kurekodi ngoma kwani kila mtu anataka kutoa kali kumshinda mwenzake, amesema Konde Boy, ambaye ndiye msanii wa kwanza kusainiwa na WCB akiachia ngoma ya Iyola.

Kwa sasa WCB ina mastaa kibao akiwemo Rayvanny, Queen Darleen, Lava Lava na Mbosso.

Advertisement