Dortmund, Schalke 04 vita yake usipime

Friday December 7 2018

 

By THOMAS NG'ITU

Dar es Salaam. Wikiendi hii katika Ligi ya Bundesliga kutakuwa na mchezo wa kukatana shoka kwa kuzikutanisha timu za Schalke 04, dhidi ya Borrusia Dortmund.
Schalke 04, watakuwa nyumbani dhidi ya Borrusia Dortmund ambao wanaongoza ligi huku wakiwa hawajapoteza mchezo wowote ndani ya Bundesliga tangu msimu huu ulipoanza. Borussia Dortmund wamefunga jumla ya mabao 37, huku Schalke wakifunga magoli 14, tu katika michezo 13, ya ligi na wanashikilia nafasi ya 12 katika msimamo wa ligi ambayo Dortmund wanaongoza.
Mchezo huo utarushwa Mubashara kupitia ST World Football HD saa11:30 jioni siku ya Jumamosi. Dortmund wanaonekana kukamilika sana katika safu ya kiungo na ushambuliaji ambayo inaongozwa na Marco Reus ambaye amaekuwa nje kwa muda akiuguza majeraha.
Reus amefunga magoli 9 na kusaidia mengine 5 huku kinara wa magoli Paco Alcacer akiwa na magoli 10 ambayo 7 kati ya hayo amefunga akitokea benchi.
Schalke 04 wanategemea kupata matokeo katika mtanange huo wa watani maarufu kama ‘River Derby’ dhidi ya kikosi imara cha Dortmund chini ya Kocha Lucian Fevre.
Kikosi hiki kiliondokewa na kiungo wao tegemeo, Leon Goretzka ambaye alitimkia Bayern mwanzoni mwa Msimu huu, hawajafanya uwekezaji wakutosha kupambana na kasi ya klabu zingine.
Wateja wa StarTimes wataweza kutizama mechi zote hizi kwa kulipia kifurushi cha Mwezi mzima cha MAMBO kwa TSH 14000 tu upande wa Antenna na SMART kwa Tsh.21000 kwa upande wa Dish.
Katika msimu huu wa sikukuu kila watakapolipia kifurushi cha MAMBO/SMART watabustiwa hadi kifurushi cha UHURU/SUPER upande wa Antenna na Dish.

Advertisement