Cheki Michongo ya kuibeba Simba

MABINGWA wa Ligi Kuu Bara, Simba jioni la leo itarejea tena Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kuvaana na Azam FC, lakini huku nyuma ikipewa michongo miwili ya maana ambayo kama wataifanyia kazi, Yanga na Azam zitabidi zisubiri sana msimu ujao.

Ndio, Wekundu hao wameshauriwa mara baada ya msimu huu kumalizika, ifanye usajili wa maana wa kiwango cha Ligi ya Mabingwa Afrika na kuwapa nafasi vijana wenye vipaji waliopo kwenye kikosi chao cMABINGWA wa Ligi Kuu Bara, Simba jioni la leo itarejea tena Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kuvaana na Azam FC, lakini huku nyuma ikipewa michongo miwili ya maana ambayo kama wataifanyia kazi, Yanga na Azam zitabidi zisubiri sana msimu ujao.ha sasa, labda tu kama itaamua kuachana nao.

Ushauri huo umekuja huku, kocha wake Patrick Aussems akiwahi kugusia mpango wake wa kuboresha kikosi chake baada ya kubaini waliteswa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwa sababu ya kutokuwa na majembe ya maana.

“Kikosi changu kinahitaji mabadiliko ya wachezaji angalau kina nafasi aongezeke mmoja, lakini kwa sasa siwezi kwani nahitaji nitimize hili la kubeba ubingwa ili mwakani tushiriki michuano ya kimataifa,” alisema Aussems alipozungumza na Mwanaspoti.

Lakini, sasa unaambiwa wakati Aussems akivuta kasi kabla ya kufanya mambo, nyota wa zamani wa klabu hiyo aliyewahi pia kukipiga Yanga na Taifa Stars, Zamoyoni Mogella alisema kama kuna kitu viongozi wa Simba hawapaswi kukifanya basi ni kuzembea kunasa wachezaji wa maana na bora Afrika.

Hata hivyo, akawaonya kuchana na mipango ya kwenda kusajili mabeki kutoka nchi za DR Congo ama Zambia, akisema viwango vyao ni vya kawaida sana.

“Kama benchi la ufundi lilikuwa makini wakati wa Ligi ya Mabingwa basi, nitashangaa kama watakwenda kusajili wachezaji kutoka AS Vita au Nkana, viwango vya timu na wachezaji wao ni kama Simba tu, hawana jipya japo walituzidi kwa umakini tu uwanjani.

Mbali na kushauri wa kutaka Simba isajili watu wa nguvu ili kula sahani moja na Al Ahly ama Mamelodi, lakini akasema viongozi na makocha lazima wawajenge kisaikolojia wachezaji na kuacha kuishi kizamani huku kuwaacha wale ambao hawako kwenye mipango yao msimu ujao.

“Kuna vijana nikiwaangalia naumia sana, wana vipaji lakini sijui wanadanganywa na viposho na pesa za mkataba wanaona bora wakakae benchi Simba, viongozi wawe washauri wazuri kwao.

“Muangalie Said Ndemla, Mohamed Ibrahim na Mzamiru Yasin hawapati sana nafasi, hawa waondoke tu watafute timu zitakazowapa nafasi ya kucheza na kuboresha viwango,” alisema.

Naye straika wa zamani wa Simba, Emmanuel Gabriel aliionya Simba kuacha kujilinganisha na klabu za ndani, ili kufahamu wanapaswa kusimama mahali gani. Alisema Simba kwa sasa iko anga za juu kabisa hivyo, ni muhimu kujilinganisha zaidi na timu kubwa Afrika na hapo watafanya usajili wa maana kwa kuleta wachezaji wenye viwango.

Hata hivyo, Gabriel ambaye ni mfungaji wa zamani wa Nazareth ya Njombe, alidai kushangaz wa na wasimamizi wa haki za akina Ndemla kuwaacha wachezaji kuendelea kuua vipaji wenye benchi la Simba, wakati wana uwezo wa kuwatafutia timu sahihi za kuwapa nafasi ya kucheza.

“Inashangaza sana kwa mchezaji mwenye kiwango kizuri, lakini unakubali kukaa benchi bila kucheza. Nimecheza Simba kwa mafanikio, naipenda na natamani ifanye makubwa. Hapa Tanzania kuna Yanga ama Azam huko Ndemla anaweza kwenda na kucheza kwa mafanikio, sijui meneja wake anawaza nini,?” alihoji.