Bocco aanza na moto Afrika Kusini

Muktasari:

Ni baada ya MCL Digital kumshuhudia akipunguza muda wake wa mapumziko na kufanya mazoezi binafsi kabla ya kuungana na wenzake.

NAHODHA na mshambuliaji wa Simba, John Bocco 'Adebayor' inaonyesha anataka kufanya mambo adimu msimu huu kutokana na kazi anayoifanya hapa Afrika Kusini.
Ni baada ya MCL Digital kumshuhudia akipunguza muda wake wa mapumziko na kufanya mazoezi binafsi kabla ya kuungana na wenzake.
Kwa kawaida Simba wanafanya mazoezi yao ya jioni saa 10:00 asubuhi kwa Tanzania saa 11:00 asubuhi, lakini yeye anaanza saa 9:00 alasiri (10:00 Tanzania) ambapo anajifua gym.
"Naenda kwanza gym kujiweka sawa baada ya hapo ndio nitaungana na wenzangu,"anasema Bocco huku akielekea gym.
Kutokana na kitendo hicho, inaonysha wazi mshambuliaji huyo ambaye msimu uliopita alionyesha kiwango cha juu hasa katika kutoa pasi za mwisho na mabao na kuisaidia timu yake kumaliza wakiwa mabingwa.