Bahanuzi apambana kurejea dimbani

Friday July 12 2019

 

By Olipa Assa

PAMOJA na kupata umaarufu mkubwa akiwa ndani ya Yanga, Said Bahanuzi amekiri jinsi ambavyo imekuwa ngumu kwake kupata timu ya kuichezea msimu ujao.
Bahanuzi baada ya kuachana na Yanga, alirejea timu yake ya zamani ya Mtibwa Sugar, alipomaliza mkataba wake alikaa nyumbani kutokana na kusumbuliwa na majeraha.
Amesema kwamba amekuwa akipata changamoto ya kuaminiwa na timu za Ligi Kuu Bara, kwa sababu hajacheza muda mrefu kutokana na majeraha.
"Unapata dili kirahisi ukiwa kazini nje na hapo ni ngumu kwani wahusika wanakuwa hawajui uwezo wako hilo ndilo ninalolipitia mimi kwa sasa, wengi wanauliza msimu ulioisha ulikuwa na timu gani.
" Hainikatishi tamaa nazidi kupambana, naamini  nikirejea uwanjani nitakuwa na kitu cha kufanya ambacho msimu mwingine utakuwa rahisi kwangu kupata timu kwani ndio maisha ya soka yalivyo," anasema Bahanuzi.
Mwaka 2012, Bahanuzi akiwa na Yanga aliibuka Mfungaji Bora wa Kombe la Kagame akifunga magoli sita.

Advertisement