Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zidane mambo mazuri Ufaransa

ZIDANE Pict

Muktasari:

  • Kiungo huyo wa zamani wa Ufaransa, mwenye umri wa miaka 53, amekuwa hana kazi tangu alipoachana na Real Madrid mwishoni mwa msimu wa 2020/21.

PARIS, UFARANSA: ZINEDINE Zidane ameripotiwa kuweka sawa hatima yake ya baadaye kwenye kazi ya ukocha.

Kiungo huyo wa zamani wa Ufaransa, mwenye umri wa miaka 53, amekuwa hana kazi tangu alipoachana na Real Madrid mwishoni mwa msimu wa 2020/21.

Sasa amefikia makubaliano ya kupewa majukumu mapya kwa mujibu wa Diario AS, na uteuzi wake utafanyika muda wowote kuanzia sasa.

Ripoti inafichua Zidane yupo kwenye orodha ya kuwa kocha ajaye wa Ufaransa, timu ambayo aliitumikia kwenye mechi zaidi ya 100 alipokuwa mchezaji.

ZIDA 01

Kocha wa sasa wa Les Bleus, Didier Deschamps alishatangaza huko nyuma kwamba dhamira yake ni kung’atuka kwenye kazi ya kuinoa timu hiyo baada ya fainali za Kombe la Dunia 2026.

Deschamps amesema: “Mwaka 2026 utakuwa mwisho. Akilini mwangu hilo lipo wazi. Nimemaliza muda wangu, nikiwa na dhamira ileile ya kuifanya Ufaransa kuwa juu muda wote, lakini 2026 utakuwa muda mzuri wa kuondoka.”€

Kama hilo lisemwalo litakuwa kweli, basi Zidane atakuwa na uhakika wa kwenda kuchukua mikoba. Deschamps alichukua mikoba ya kuinoa Ufaransa mwaka 2013 na amebeba mataji ya kutosha kwenye timu hiyo, akiongoza kubeba taji la Kombe la Dunia 2018 na kufika fainali pia ya Kombe la Dunia 2022 na ilipoteza mbele ya Argentina.

Lakini, Zidane, ambaye alishinda Kombe la Dunia 1998 akiwa kama mchezaji, alifanya vizuri kama kocha kwenye kikosi cha Real Madrid na alibeba mataji ya kutosha, ikiwamo Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa misimu mitatu mfululizo.