Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zamalek farao mpya, Al Ahly mambo magumu

ZAMALEK Pict
ZAMALEK Pict

Muktasari:

  • Zamalek wametwaa ubingwa huo licha ya kuwa na changamoto za kifedha, kuzuiwa kusajili usajili, na kucheleweshwa kwa mishahara kwa wachezaji wake wakati wa msimu huu.

CAIRO, MISRI: Zamalek SC wametangazwa kuwa Mafaroa wapya wa Ligi Kuu ya Misri kwa mara ya 15 katika historia yao baada ya kuifunga Ceramica Cleopatra bao 1-0 katika mchezo wa mwisho wa msimu huu.

Ubingwa huo wa Zamalek wa kwanza tangu alipotwaa kwa mara ya mwisho 2022, pia wamehakikisha nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2026/2027, ikiwa ni kurejea kwao kwenye mashindano hayo baada ya kukosekana kwa misimu mitatu mfululizo huku watani wao wa jadi Al Ahly rasmi itashiriki Kombe la Shirikisho Afrika.

Zamalek walimaliza kileleni mwa msimamo kwa pointi 56, wakifuatiwa na Pyramids FC waliokuwa na pointi 54, huku Al Ahly wakimaliza nafasi ya tatu kwa pointi 53 katika mbio kali za ubingwa zilizodumu hadi mechi ya mwisho ya msimu.

ZAMA 02

Zamalek wametwaa ubingwa huo licha ya kuwa na changamoto za kifedha, kuzuiwa kusajili usajili, na kucheleweshwa kwa mishahara kwa wachezaji wake wakati wa msimu huu.

Katika mchezo mwingine, Al Ahly waliokuwa na wachezaji 10 waliifunga Al Masry SC mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria katika mchezo wa mwisho wa ligi siku ya Jumatano, lakini ushindi huo haukuwasaidia kupanda zaidi ya nafasi ya tatu, hivyo kufuzu kucheza Kombe la Shirikisho msimu ujao.

Winga Mahmoud Hassan aliipa Ahly mwanzo mzuri kwa kufunga bao la mapema dakika ya pili kupitia shuti kali akiwa ndani ya eneo la hatari.

Al Ahly walibaki na wachezaji 10 dakika ya 38 baada ya beki Yassin Marei kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kumuangusha mshambuliaji wa Masry, Mounder Temine, aliyekuwa akielekea golini.

ZAMA 01

Licha ya upungufu huo wa wachezaji, Ahly walijilinda vizuri na kuthibitisha ushindi wao dakika ya 89 kupitia penalti iliyofungwa na Trezeguet, aliyefunga bao lake la pili katika mchezo huo.

Hata hivyo, ushindi huo haukubadilisha nafasi yao kwenye msimamo baada ya msimu usioridhisha ambapo klabu hiyo ilikosa mataji yote makubwa isipokuwa Kombe la Super Cup la Misri.

Mabingwa hao wa Afrika mara 12 sasa watashiriki Kombe la Shirikisho CAF baada ya kushindwa kufuzu Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2003.

ZAMA 03

Tangu kuanzishwa kwa mashindano ya Kombe la Shirikisho mwaka 2004, Al Ahly wamewahi kushiriki mara moja pekee mwaka 2014 baada ya kushuka kutoka Ligi ya Mabingwa na waliweza kutwaa ubingwa wa mashindano hayo.

Hili ni pigo kubwa kwa Al Ahly ambao waliondolewa kwenye hatua za mtoano Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kutawala kwa miaka kadhaa.

Hata hivyo, inaelezwa kuwa mabosi wa timu hiyo wanataka kususia kucheza Kombe la Shirikisho Afrika bila kueleza sababu za msingi za kufanya jambo hilo ambalo linaweza pia kuwafanya CAF wakawapiga faini au kuwafungia muda mrefu.