Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Winga Super Eagles astaafu soka

MUSSA Pict

Muktasari:

  • Uamuzi wa nyota huyo mwenye umri wa miaka 33 unakuja siku chache tu baada ya nahodha wa muda wa Super Eagles, William Troost-Ekong, naye pia kutangaza kustaafu kuitumikia timu ya taifa ya mabingwa mara tatu wa Afrika.

NYOTA aliyecheza mechi nyingi zaidi katika historia ya timu ya taifa ya Nigeria, Ahmed Musa ametangaza kustaafu soka la kimataifa.

Uamuzi wa nyota huyo mwenye umri wa miaka 33 unakuja siku chache tu baada ya nahodha wa muda wa Super Eagles, William Troost-Ekong, naye pia kutangaza kustaafu kuitumikia timu ya taifa ya mabingwa mara tatu wa Afrika.

Uamuzi wa Musa umechangiwa na kuachwa kwake katika kikosi cha Nigeria kitakachoshiriki Kombe la Mataifa ya Afrika 2025 (AFCON), litakaloanza Desemba 21 Morocco, ikitarajia kuanza kuvaana na Tanzania katika mechi yua Kundi C lenye timu za Tunisia na Uganda pia.

“Ndugu Wanigeria, familia ya Super Eagles. Baada ya tafakari kubwa, nimeamua kustaafu soka la kimataifa, na hivyo kufunga safari ya karibu miaka 15 nikiwa na Super Eagles,” Musa aliandika kwenye ujumbe mrefu kwenye mitandao ya kijamii.

“Kuanzia mwito wangu wa kwanza kabisa, kuivaa jezi ya kijani na nyeupe kulimaanisha kila kitu kwangu. Nilikuwa kijana mdogo sana wakati safari ilipoanza.

MUs 01

“Nakumbuka niliitwa kwa wakati mmoja timu za U20, U23 na Super Eagles. Nilikuwa mdogo, bado najifunza na nikisafiri mara kwa mara, lakini sikuwahi kulalamika.

“Kila mara Nigeria iliponihitaji, nilijitokeza. Haikuwa jambo la kufikiria mara mbili.”

Musa alipata umaarufu kupitia kiwango kizuri alichokuwa nacho katika klabu ya Ligi Kuu ya Nigeria, Kano Pillars, baada ya kuwakilisha taifa katika ngazi za vijana.

Alianza kuitumikia timu ya taifa Septemba 5, 2010 akiwa na umri wa miaka 17 tu, akaingia kama mbadala wa John Obi Mikel katika mechi ya kufuzu AFCON 2012 dhidi ya Madagascar, ambayo Nigeria ilishinda kwa mabao 2-0.

Musa alifunga bao lake la kwanza la kimataifa Machi 2011 katika mechi ya kirafiki dhidi ya Kenya.

“Soka lilinipeleka sehemu nyingi duniani, lakini Nigeria daima ilikuwa nyumbani. Kucheza mechi 111 kwa ajili ya nchi yangu ni jambo ninaloliheshimu sana,” aliendelea kusema.

“Kuwa mchezaji aliyocheza mechi nyingi zaidi katika historia ya soka la Nigeria ni heshima kubwa. Kila nilipoivaa jezi, nilielewa uzito wa jukumu hilo.

“Nilijitahidi kutoa kila nilichokuwa nacho, iwe mambo yalikuwa mazuri au magumu, kwa sababu kuitumikia Nigeria ilikuwa kubwa kuliko mimi mwenyewe.”

Musa aliitumikia Nigeria kwa miaka 15 na akawapita Vincent Enyeama na Joseph Yobo kuwa mchezaji aliyocheza mechi nyingi zaidi, akiwa na mechi 111.

MUs 02

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Leicester City na CSKA Moscow alicheza mechi muhimu katika ushindi wa Nigeria wa AFCON 2013 na pia anashikilia rekodi ya kuwa Mfungaji Bora wa Nigeria katika historia ya Kombe la Dunia la FIFA.

“Kuna nyakati sitazisahau kamwe. Ushindi wa AFCON 2013 utaendelea kuwa wa kipekee. Timu ilionyesha maana halisi ya kuichezea Nigeria,” aliongeza.

“Kufunga mabao Kombe la Dunia dhidi ya Argentina na Iceland ni kumbukumbu nitakazobeba milele. Kufunga mabao manne Kombe la Dunia na kuwa mfungaji bora wa Nigeria katika mashindano hayo ni jambo ninalolishukuru sana.

“Kuwa nahodha wa Super Eagles kulikuwa sehemu muhimu ya safari yangu. Kuvaa kitambaa cha unahodha kulinifundisha mengi kuhusu uwajibikaji, subira na kuwaweka wengine mbele.

“Haikuwa kuhusu kuongoza, bali kusaidia timu, kuwaunga mkono wachezaji vijana na kulinda heshima ya jezi. Hata katika nyakati ngumu na ukosoaji, dhamira yangu kwa Nigeria haikubadilika.

“Soka lilinipa kazi, lakini Nigeria ilinipa maana ya maisha. Kwa wenzangu wa timu kwa miaka yote, makocha, wafanyakazi wa benchi la ufundi na viongozi, asanteni kwa kuniunga mkono.

“Kwa mashabiki walioko nyumbani na ughaibuni, viwanjani na mbele ya runinga, msaada wenu ulimaanisha zaidi kuliko mnavyodhani. Ninapoondoka kwenye soka la kimataifa, ninaondoka kwa amani na shukrani. Najua nilitoa kilicho bora zaidi.

“Najua Super Eagles itaendelea kusonga mbele. Na najua uhusiano huu hautakatika kamwe. Mara Tai, daima Tai.”