Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Winga Real Madrid na Everton, Drenthe, apata kiharusi

WINGA Pict

Muktasari:

  • Mchezaji huyo wa kimataifa wa zamani wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 38, alilazwa hospitalini siku ya Ijumaa Oktoba 17, 2025.

Winga wa zamani wa Real Madrid na Everton, Royston Drenthe, amelazwa hospitalini baada ya kupata kiharusi.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa zamani wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 38, alilazwa hospitalini siku ya Ijumaa Oktoba 17, 2025.

Taarifa hiyo imetolewa na FC de Rebellen, shirika linalowakilisha wachezaji wa zamani wa soka akiwamo Drenthe.

Taarifa hiyo imesomeka: “Ijumaa iliyopita, Royston Drenthe alipata kiharusi.

WING 01

Drenthe kwa sasa anapata matibabu mazuri na yuko mikononi mwa wataalamu. Timu na wote wanaohusika wanatamani apone haraka.”

Drenthe alianza maisha yake ya soka katika klabu ya Feyenoord kabla ya kujiunga na Real Madrid mwaka 2007, ambako alishinda taji la La Liga mwaka uliofuata.

Alitolewa kwa mkopo kujiunga na Everton msimu wa 2011–2012, na baadaye kuchezea klabu zingine ikiwamo Reading na Sheffield Wednesday.

WING 02

Kupitia ukurasa wao wa X (zamani Twitter), Everton wametoa salamu za pole wakisema: “Kila mmoja ndani ya Everton anatuma salamu za pole na kumtakia Royston Drenthe afya njema na uponyaji wa haraka baada ya ripoti kwamba amelazwa hospitalini.”