Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kadi nyekundu yamuibua Maresca, ang’ata na kupuliza

CHELSEA Pict

Muktasari:

  • Kadi ya pili ya njano ya Gusto katika dakika za mwisho za mechi dhidi ya Nottingham Forest ilifanya idadi ya wachezaji watano wa Chelsea kuonyeshwa kadi nyekundu katika mechi sita za mwisho.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Chelsea, Enzo Maresca, alikosoa kadi nyekundu aliyoonyeshwa staa wake Malo Gusto, lakini pia alimsifu kwa kuchukua uamuzi uliosababisha kadi hiyo.

Kadi ya pili ya njano ya Gusto katika dakika za mwisho za mechi dhidi ya Nottingham Forest ilifanya idadi ya wachezaji watano wa Chelsea kuonyeshwa kadi nyekundu katika mechi sita za mwisho.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa alimfanyia faulo staa wa Forest, Neco Williams, aliyekuwa akijaribu kuanzisha shambulizi katika dakika ya 87.

Maresca ambaye hakuwapo katika benchi kutokana na adhabu aliyopewa baada ya mechi dhidi ya Liverpool, amesema kadi nyekundu kama zile zinaweza kuepukika, hususani katika dakika za mwisho lakini jambo zuri ni kwamba mchezaji alikuwa anaonyesha kwamba hataki kuruhusu mpinzani aende katika lango kwa namna yoyote.

CHELS 01

"Hakutaka kuona timu inaruhusu bao, alipambana kuhakikisha timu inashinda, lakini zaidi pia hairuhusu bao. Ni jambo zuri kuwa na aina hiyo ya matamanio, lakini kuna muda unaona kabisa haikuwa na maana sana," amesema Maresca.

Mabao kutoka kwa Josh Acheampong, Pedro Neto na Reece James yaliipeleka Chelsea katika nafasi ya sita kwenye msimamo wa EPL ikiwa imecheza mechi nane, imeshinda nne, sare mbili na kufungwa mbili huku ikiwa na pointi 14 ikiwa ni tofauti ya pointi tano nyuma ya Arsenal ambayo inaongoza ligi ikiwa na pointi 19.

Chelsea itarudi nyumbani kucheza dhidi ya Sunderland wikiendi ijayo kabla ya kuvaana na Spurs katika dabi ya London, Novemba 1.

CHELS 02

Mbali ya mechi hii ya Jumamosi iliyopita, siku hiyo pia kulikuwa na mechi nyingine sita ambapo, Wolves iliendelea na hali yake mbaya ikicheza mechi ya nane bila ya kupata ushindi wowote baada ya kupoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya Sunderland ambayo imeendelea kuonyesha makali tangu ipande daraja msimu huu ikiwa imefikisha pointi 14 na kupanda hadi nafasi ya saba katika msimamo.

Brighton ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Newcastle United na kufikisha pointi 12, ikisogea hadi nafasi ya tisa.

Vijana wa Mikel Arteta walipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Fulham na kuendelea kujikita zaidi kileleni katika msimamo wa ligi.

Manchester City iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Everton ikifikisha pointi 16 na kuendelea kujisogeza kimya kimya katika mbio za kuwania taji la Ligi Kuu England msimu huu.

Burnley pia ilishinda mechi yake ya pili ya ligi kwa kuichapa Leeds United mabao 2-0.