Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watatu Liverpool kuikosa Chelsea kesho

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  • Wachezaji wengine waliotajwa na kocha huyo ni Hugo Ekitike na Federico Chiesa, ambao wanakabiliwa na majeraha, licha ya kutegemewa kwa ripoti ya mwisho ambayo itathibitisha kama wataweza kuwa sehemu ya kikosi cha Liverpool hapo kesho ama la.

KOCHA wa Liverpool, Arne Slot amethibitisha kuwa mlinda mlango Alisson Becker hatakuwepo kwenye mechi ya EPL dhidi ya Chelsea itakayopigwa kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.

Wachezaji wengine waliotajwa na kocha huyo ni Hugo Ekitike na Federico Chiesa, ambao wanakabiliwa na majeraha, licha ya kutegemewa kwa ripoti ya mwisho ambayo itathibitisha kama wataweza kuwa sehemu ya kikosi cha Liverpool hapo kesho ama la.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kabla ya mechi hiyo, Slot amefichua kuwa Alisson atakuwa nje hadi wiki tatu, na hatasafiri kwenda kujiunga na timu ya taifa ya Brazil kwa ajili ya mechi za kimataifa za kirafiki dhidi ya Korea Kusini na Japan wiki ijayo.

"Alisson hatakuwa sehemu ya kikosi kesho na hatasafiri kwenda Brazil. Hugo Ekitike atafanya mazoezi tena leo, na hali ni hiyo hiyo kwa Federico Chiesa.

Kuhusu Alisson, sijafahamu kama ataweza kurudi kwenye kikosi baada ya mapumziko ya kimataifa lakini hilo linategemea na maendeleo ya afya yake."

Slot ameongeza kuwa, licha ya kuwakosa wachezaji hao kuelekea mechi ya kesho dhidi ya Chelsea, benchi lake la ufundi halina wasiwasi, kwani wamejiandaa vizuri na ana Imani kubwa atapambana na kupata ushindi.

Alisson alikosa mechi 26 msimu uliopita kutokana na maumivu ya msuli wa paja (hamstring), na pia alikosa mechi 15 msimu wa 2023/24 kwa tatizo hilo hilo.

Kwa mujibu wa ripoti ya The Athletic ya jana Alhamisi, Oktoba 2, 2025, Allisson anatarajiwa kuwa nje hadi kwa wiki sita, na atakosa angalau mechi nane, akianza mechi ya kesho dhidi ya Chelsea.