Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pigo Liverpool, Alisson kuikosa Chelsea Jumamosi

Muktasari:

  • Kutokana na kuumia huko, Kocha wa Liverpool, Arne Slot, amesema Alisson atakosa mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Chelsea itakayochezwa Jumamosi wiki hii.

KIPIGO cha bao 1-0 ilichopata Liverpool kutoka kwa Galatasaray kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, kimeongeza maumivu mara mbili baada ya kipa namba moja wa kikosi hicho, Alisson Becker kuripotiwa kupata majeraha yanayomfanya kuikosa mechi ijayo.

Kutokana na kuumia huko, Kocha wa Liverpool, Arne Slot, amesema Alisson atakosa mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Chelsea itakayochezwa Jumamosi wiki hii.

Kipa huyo mwenye umri wa miaka 32, alilazimika kuondolewa uwanjani dakika ya 56 na nafasi yake kuchukuliwa na Giorgia Mamardashvili kwenye kipigo cha 1-0 mjini Istanbul.

Alisson alionekana akichechemea baada ya kuokoa shuti la mfungaji Victor Osimhen, huku mshambuliaji Hugo Ekitike naye akiumia baada ya kujinyoosha kufuata mpira na kulazimika kuondolewa.

Slot alisema kipa huyo wa kimataifa wa Brazil aliyecheza jumla ya mechi 235 za Ligi Kuu England ndani ya Liverpool, alihisi kitu alipokuwa akikimbia kurudi nyuma.

"Kama mchezaji wangu amelala chini mara tisa kati ya kumi huwa nahisi hali mbaya, na ninaposema mbaya namaanisha kuwa hawezi kuendelea," amesema Slot.

"Sio dalili nzuri kuondoka uwanjani kwa namna hiyo. Ni dhahiri hatacheza Jumamosi."

Mamardashvili sasa ana nafasi ya kucheza mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu England ugenini Stamford Bridge. Mlinda mlango huyo wa Georgia alisajiliwa kutoka Valencia majira ya kiangazi kwa dau la pauni milioni 29.

Msimu uliopita, Alisson alikosa mechi 10 za Ligi Kuu England kutokana na majeraha ya msuli wa paja (hamstring).

Kuna wasiwasi pia kuhusu Ekitike, ambaye alilazimika kutoka kipindi cha pili.

"Sikuwa nafikiria kama tuna jeraha, lakini Hugo alihisi kitu," Slot ameongeza.

"Alisema hawezi kuendelea, hivyo tukalazimika kumtoa. Tutaona hali yake itakuwaje kuelekea mwishoni mwa wiki."

Liverpool ndio vinara katika msimamo wa Ligi Kuu England ikikusanya pointi 15, mbili juu ya Arsenal na Crystal Palace zinazofuatia nafasi ya pili na tatu.