Wales yapewa 30%, Italia 62% kufuzu
Muktasari:
- Kikosi hicho kinachonolewa na Craig Bellamy kiliichapa North Macedonia 7-1 Jumanne iliyopita katika mchezo wa mwisho wa kufuzu fainali za Kombe la Dunia na hivyo kufanikiwa kuingia kwenye nusu fainali ya mchujo wa kusaka tiketi ya michuano hiyo.
ZURICH, USWISI: WALES imepewa nafasi ya asilimia 30 ya kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia 2026.
Kikosi hicho kinachonolewa na Craig Bellamy kiliichapa North Macedonia 7-1 Jumanne iliyopita katika mchezo wa mwisho wa kufuzu fainali za Kombe la Dunia na hivyo kufanikiwa kuingia kwenye nusu fainali ya mchujo wa kusaka tiketi ya michuano hiyo.
Lakini, nafasi yao ya kwenda kuungana kwenye fainali za Marekani, Canada na Mexico, itapaswa kuichapa Bosnia and Herzegovina kwenye mechi yao ya nusu fainali ya mchujo Machi 26.
Na baada ya hapo, huenda ikacheza fainali dhidi ya Italia, la kama Northern Ireland itakuwa imekichapa kikosi cha Azzurri katika nusu fainali nyingine ya mchujo huo.
Wales ilimaliza nafasi ya pili kwenye Kundi J la kufuzu fainali hizo baada ya kukusanya pointi 16, mbili tu nyuma ya vinara Ubelgiji. Ilishinda mechi tano, sare moja na kupoteza mbili na ilionekana kama kuivimbia Ubelgiji baada ya mechi zao kumalizika kwa kipigo cha 4-3 na 4-2.
Lakini, utabiri wa kompyuta umeipa Wales asilimia 30 tu ya uwezekano wa kufuzu fainali hizo. Kwenye mchakato huo, Italia imepewa asilimia 62 ya uwezekano wa kufuzu fainali hizo, wakati Northern Ireland imepewa asilimia 3.8, huku ikiwa na mtihani wa kuikabili Italia kwenye nusu fainali ya mechi hizo za mchujo.
Republic of Ireland yenyewe imepewa asilimia 8.4 ya uwezekano wa kufuzu fainali hizo, ambapo mechi yao ya mchujo itakipiga na Czech Republic. Timu yenyewe nafasi finyu zaidi ni North Macedonia yenye asilimia 3.2. Wales bado inaamini itafuzu kwa fainali hizo za Kombe la Dunia licha ya kukabiliwa na njia ngumu katika kufikia michuano hiyo.
Kocha Bellamy amesema kiwango cha vijana wake kipo kwenye ubora mkubwa, hivyo ni mechi hizo za mchujo wanazitazama kama njia muhimu ya kufikia kwenye fainali hizo.