Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waarabu warudi upya kwa Mo Salah

Muktasari:

  • Fowadi huyo wa kimataifa wa Misri alisaini mkataba mpya wa kuitumikia miamba hiyo ya Anfield hadi majira ya kiangazi 2027.

LIVERPOOL, ENGLAND: KLABU za Saudi Arabia tayari zimeanza mchakato wa kumnasa supastaa wa Liverpool, Mohamed Salah.

Fowadi huyo wa kimataifa wa Misri alisaini mkataba mpya wa kuitumikia miamba hiyo ya Anfield hadi majira ya kiangazi 2027.

Lakini, hatima ya Mo Salah huko Anfield yapo kwenye wasiwasi mkubwa baada ya kuwekwa benchini na kocha Arne Slot katika mechi mbili za mwisho ilizocheza Liverpool. Jambo hilo limemfanya beki wa zamani wa Liverpool, Jamie Redknapp aamini kwamba Mo Salah anaweza kufikiria kuachana na timu hiyo kama mambo yatashindwa kubadilika.

Ni wazi uhamisho huo utasubiri hadi kwenye dirisha la Januari, lakini klabu kadha tayari zimeanza kuhusishwa na mshambuliaji huyo. Na sasa haizuiliki kwa taarifa za kutoka Saudi Arabia klabu za kutoka huko Mashariki ya Kati zinapiga hesabu za kwenda kunasa saini yake.

Ripoti zinafichua klabu za Saudi Pro League zipo kwenye hali nzuri ya kiuchumi kuwezesha uhamisho wa Mo Salah na bila shaka mchezaji huyo atakuwa tayari kuachana na Liverpool. Mwaka 2023 klabu ya Al-Ittihad iliripotiwa kuhitaji saini ya mchezaji huyo ili akakipige Mashariki ya Kati.

"Nilidhani kuna fursa muhimu ya kwenda kujiunga Saudi Pro League," alisema Salah huko nyuma alipozungumzia uwezekano wa kwenda Saudi Arabia.

"Niliamini ningekwenda kama nisingesaini mkataba mpya Liverpool. Uhusiano wangu na watu wa huko Saudi Arabia bado upo vizuri. Kulikuwa na mazungumzo siriazi kwa ajili ya kunisajili."

Klabu za Saudi Arabia zilizopo chini ya Public Investment Fund bado zina pesa za kutosha za kutumia baada ya kufungulia pochi kunasa huduma za masupastaa kibao waliokuwa wakitamba kwenye ligi za Ulaya ili kwenda kucheza kwenye ligi ya Saudi Pro League.

MASTAA WA SOKA WALIOTUA SAUDI PRO LEAGUE MIAKA YA KARIBUNI

-Cristiano Ronaldo - Al Nassr

-Sadio Mane - Al Nassr

-Joao Felix - Al Nassr

-Riyad Mahrez - Al Ahli

-Roberto Firmino - Al Ahli

-Fabinho - Al Ittihad

-Edouard Mendy - Al Ahli

-N'Golo Kante - Al Ittihad

-Pierre-Emerick Aubameyang - Al Qadsiah