Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waarabu wakomaa kumng’oa Mo Salah

RIYADH SAUDI ARABIA. AL-Ittihad ya Saudi Arabia imeripotiwa kuwa na uhakika wa kunasa saini ya supastaa wa Liverpool, Mohamed Salah kabla ya dirisha la kufungwa.

Na kama dili hilo litatiki, basi Mo Salah atakuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani, akimpiku kwa mshahara, supastaa wa Kireno, Cristiano Ronaldo. Al-Ittihad ipo tayari kumpa winga huyo wa Misri ofa ya mshahara itakayozidi ule anaolipwa Ronaldo huko Al-Nassr wa Pauni 173 milioni, huku wakilenga kuwalipa Liverpool ada ya uhamisho ya Pauni 86 milioni.

Kwa sasa, Ronaldo, ndiye mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani, huku akifanywa kama nembo ya Saudia.

Dili la mkali huyo wa zamani wa Manchester United linamshuhudia akilipwa Pauni 3.4 milioni kwa wiki na atakuwa anakunja mkwanja huo hadi Juni 2025.

Mshindi wa sasa wa Ballon d’Or, Karim Benzema yupo kwenye namba mbili akiwa analipwa Pauni 3.3 milioni kwa wiki, huku Neymar akiwa kwenye namba tatu kwa kulipwa Pauni 2.5 milioni kwa wiki baada ya kutua Al-Hilal kwa ada ya Pauni 77.6 milioni akitokea Paris Saint-Germain. Lakini, kama Mo Salah atatua Saudia, basi atavuna pesa nyingi kuzidi mastaa wote waliotajwa hapo juu. Na kinachoelezwa, klabu hiyo ya Saudia ina uhakika itanasa saini ya staa huyo kwenye umri wa miaka 31 kabla ya dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi kufungwa.

Mwandishi wa habari, Rudy Galetti alisema: “Al Ittihad hawatakata tamaa kwa Salah. Wametuma ofa kubwa sana kumshawishi hasa Klopp (Jurgen) - ambaye bado anapingana na ishi ya kumwaachia aondoke.”