Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Ufaransa afiwa, kuondoka kambini kwa muda

Muktasari:

  • Deschamps baada ya kupata taarifa hizo sasa atalazimika kuondoka kwa muda kwenye kambi hiyo ,alirejea kwao Ufaransa kufungana na familia yake pamoja na kumuaga mama yake.

Kambi ya timu ya Taifa ya Ufaransa imepata pigo baada ya kocha wake mkuu Didier Deschamps kufiwa na mama yake mzazi Marie Borda.

Deschamps baada ya kupata taarifa hizo sasa atalazimika kuondoka kwa muda kwenye kambi hiyo ,alirejea kwao Ufaransa kufungana na familia yake pamoja na kumuaga mama yake.

Maamuzi hayo yatamfanya kocha huyo kuukosa mchezo wa mwisho wa makundi dhidi ya Norway utakaopigwa Juni 26.2026.

"Kocha wa timu ya taifa alihuzunishwa sana kujua asubuhi ya leo kuhusu kifo cha mamake,” imesema taarifa ya Shirikisho la Soka la Ufaransa (FFF).

Hata hivyo kocha huyo amefanya uamuzi wa kumuachia msaidizi wake wa kwanza Guy Stephan kusimamia majukumu yote wakati ambao hatakuwa kwenye kambi hiyo.

"Kwa makubaliano na Philippe Diallo, Rais wa Shirikisho la Soka la Ufaransa, ambaye yuko kwenye kambi ya mazoezi ya timu ya taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps amemkabidhi msaidizi wake, Guy Stephan, jukumu la kukiongoza kikosi hadi atakaporejea.

Deschamps (57) ni mmoja wa makocha waliokaa muda mrefu katika kuifundisha Ufaransa tena kwa mafanikio  ,tangu alipoteuliwa kushika nafasi hiyo mwaka 2012.