Waandishi wa habari wakiona cha moto kwa Ronaldo

Muktasari:

Ronaldo, ambaye kwa sasa analalamikiwa na wadau wa soka kwa kuwa  na ukame wa mabao alifunga mabao mawili katika mchezo huo lakini hakuwa tayari kuzungumza na waandishi wa habari.

MADRID, HISPANIA. NYOTA wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amewalipukia waandishi wa habari ambao walitaka kufanya naye mahojiano baada ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya APOEL ambapo kikosi cha Hispania kilipata jumla ya mabao 6-0.
Ronaldo, ambaye kwa sasa analalamikiwa na wadau wa soka kwa kuwa  na ukame wa mabao alifunga mabao mawili katika mchezo huo lakini hakuwa tayari kuzungumza na waandishi wa habari.
Baaada ya mechi waandishi wa habari walimfuata na aliwajibu kwa ukali; “Mnataka nisema nini. Nawezaje kuongea na nyie kitu fulani halafu kesho nakuta mambo yaliyoandikwa ni mengine.”
Lakini wachambuzi wa masuala ya soka wanasema kwamba Ronaldo alishindwa kuzungumza kwa kuwa alihofia kuulizwa kuhusu mwenendo wake katika klabu kwa siku za karibuni.