Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vita ya PFA yazidi kupamba moto EPL 2025/26

Muktasari:

  • Kuna majina mengi yanayotajwa katika kundi la mastaa wa timu 20 zinazoshiriki ligi hiyo yenye wachezaji 528. Vikosi hivyo vina hadi wachezaji 17 wasio raia wa nchi hiyo (non-homegrown) kwa kila timu, huku jumla ya wachezaji wa kigeni ikiwa 380, wakichangia takriban asilimia 72 ya nyota wote wa ligi hiyo.

IPSWICH, ENGLAND: WAKATI ukitafakari ulivyomalizika mzunguko wa 32 wa Ligi Kuu England, jana kwa mechi moja kati ya Manchester United dhidi ya Leeds United iliyopigwa Old Trafford, wachambuzi wa soka nchini humo wameanza kubishana juu ya staa gani ataibuka mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa EPL (PFA), msimu wa 2025/26 utakapomalizika Mei 24, mwaka huu.

Kuna majina mengi yanayotajwa katika kundi la mastaa wa timu 20 zinazoshiriki ligi hiyo yenye wachezaji 528. Vikosi hivyo vina hadi wachezaji 17 wasio raia wa nchi hiyo (non-homegrown) kwa kila timu, huku jumla ya wachezaji wa kigeni ikiwa 380, wakichangia takriban asilimia 72 ya nyota wote wa ligi hiyo.

Sasa basi wakati ukitafakari hayo, mjadala wa PFA Mchezaji Bora wa 2025/26 umeshika kasi, lakini kuna takriban majina matano yanayotawala kwa sasa, huku nahodha na kiungo wa Manchester United, Bruno Fernandez akiongoza akifuatiwa kwa karibu na kiungo wa Arsenal, Declan Rice, beki wa Manchester, City Rayan Cherki na mshambuliaji wa timu hiyo, Antoine Semenyo. 

Vilevile kuna straika mwingine wa Man City, Erling Haaland na beki wa kati wa Arsenal, Gabriel Magalhaes.

Sahau kuna Bruno na Rice, mgombea mwingine anayestahili zaidi wa tuzo ya PFA Mchezaji Bora wa Mwaka ni Cherki

angalau hivyo ndivyo wachambuzi maarufu wa Kiingereza wa talkSPORT wanavyoamini.

BRUNO FERNANDEZ

Bruno na Rice wote wamekuwa wachezaji muhimu kwa klabu zao za Manchester United na Arsenal msimu huu.

Na kwa wengi, wawili hao ni miongoni mwa wagombea wakuu wa tuzo hiyo binafsi ya mchezaji bora. Hata hivyo, kuna wengine wasiopaswa kupuuzwa akiwamo Cherki.

Cherki amekuwa mchezaji wa kuvutia Man City tangu ajiunge majira ya kiangazi, mwaka jana akitokea Lyon ya Ufaransa na mchezaji huyo Mfaransa ameandikisha asisti nane na kufunga mabao matatu katika kikosi cha Pep Guardiola kwenye Ligi Kuu msimu huu.

Hata hivyo, kuna zaidi katika mchezo wa Cherki ambayo wachambuzi hao wanaamini yanapaswa kutambuliwa wakati wa kugawa tuzo za mwisho wa msimu. Ingawa baadhi ya mashabiki wa Manchester City wanaweza kukubaliana na mtazamo huo, wengi wataamini wachezaji wengine wanastahili zaidi tuzo hiyo.

DECLAN RICE

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27 amekuwa mhimili wa Arsenal katika mbio za ubingwa akihusika moja kwa moja kwenye mabao tisa msimu huu, akifunga manne.

Pia amekuwa na mchango mkubwa eneo la kiungo kwa jumla akiwa miongoni mwa vinara wa ligi kwa kutengeneza nafasi akiwa nazo 58  pamoja na takwimu za juu za 'takolingi' (57) na kuvunja mashambulizi ya wapinzani mara 30.


BRUNO FERNANDEZ

Nahodha huyo wa Manchester United na kiungo mbunifu katika ligi. Licha ya timu yake kupitia kwenye changamoto tangu msimu wake wa kwanza, Fernandes amekuwa nguzo ya ubora Old Trafford. Anaongoza kwa asisti akiwa nazo 16, pia yupo juu kwa kutengeneza nafasi akifanya hivyo mara 101, huku zile za wazi zikiwa 24, na pasi za hatari 13.

United wanatarajiwa kurejea Ligi ya Mabingwa, na Fernandes ndiye tumaini la kuwafikisha huko.


GABRIEL MAGALHAES

Beki wa kati wa Arsenal, Gabriel Magalhaes anatafuta kuwa beki wa kwanza kushinda tuzo ya PFA Mchezaji Bora wa Mwaka tangu Virgil van Dijk wa Liverpool alipofanya hivyo 2019.

Makipa na mabeki mara chache walioingia kwenye kinyang’anyiro hicho ni wachezaji watatu tu walivuta tuzo ambao ni Paul McGrath, John Terry na Van Dijk tangu kuanzishwa kwa Ligi Kuu England 1992.

Hata hivyo, Magalhaes amekuwa sehemu ya safu bora ya ulinzi ya Arsenal iliyoruhusu mabao machache zaidi ya ligi (22), na ni miongoni mwa wachezaji 10 bora kwa kuzuia mashuti ya wapinzani akifanya hivyo mara 25.


ERLING HAALAND

Ingawa ni kama amepoa fulani kwa sasa tofauti na mwanzoni mwa ligi na licha ya kwamba anaongoza chati ya ufungaji bora, pia huwezi kumuacha kando katika kinyang'anyiro cha tuzo hiyo. Haaland amefunga mabao 22 msimu huu - zaidi kuliko mchezaji mwingine yeyote Ligi Kuu England.

Mabao hayo yametokana na mashuti 102, pia mengi kuliko mchezaji mwingine yeyote. Kama ataiongoza City kuchukua ubingwa atakuwa mgombea muhimu wa  tuzo hiyo.

ANTOINE SEMENYO

Uhamisho wake Januari kwenda Manchester City ulipishana na kushuka kwa fimu ya Haaland. Hata hivyo, Semenyo ameendeleza ubora wake kutoka Bournemouth hadi Etihad.

Amefunga mabao 15 msimu huu na matano kati ya hayo yamekuja baada ya kujiunga City. Pia ana asisti nne.


RAYAN CHERKI

Beki huyo mwenye umri wa miaka 22 ana asisti nane licha ya kuanza mechi 14 za ligi akiwa wa pili baada ya Fernandes.

Pia ni wa pili kwa kuzima mashambulizi ya wapinzani wao akifanya hivyo mara 15, na wastani wake wa pasi sahihi ni 2.9 kwa kila dakika 90.

Aidha, ana wastani wa dribo 2.5 zinazofanikiwa kwa kila dakika 90, jambo linaloonyesha ubunifu wake mkubwa.