Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vinicius, Real Madrid kunafukuta

Muktasari:

  • Baada ya kutemwa mara mbili wiki za hivi karibuni na kocha mpya Xabi Alonso, winga huyo anadaiwa kuwa anafikiria kuondoka mwisho wa msimu huu endapo Madrid haitampa mkataba mpya wenye ongezeko la mshahara ambao anataka uwe sawa na Kylian Mbappe anayepokea Euro 600,000 kwa wiki.

MADRID, HISPIANIA: MABOSI wa Real Madrid wamesisitiza kuwa hawatabadili ofa yao ya mkataba kwa fundi Vinicius Junior licha ya mvutano unaoendelea kati ya klabu hiyo ya Hispania na winga huyo wa kimataifa wa  Brazil.

Baada ya kutemwa mara mbili wiki za hivi karibuni na kocha mpya Xabi Alonso, winga huyo anadaiwa kuwa anafikiria kuondoka mwisho wa msimu huu endapo Madrid haitampa mkataba mpya wenye ongezeko la mshahara ambao anataka uwe sawa na Kylian Mbappe anayepokea Euro 600,000 kwa wiki.

Kwa mujibu wa gazeti la Marca, nafasi ya Vinicius ndani ya Madrid imebadilika sana tangu kuwasili kwa Alonso ambaye amekuwa na msimamo tofauti akihitaji aonyeshe kiwango bora mazoezini na hakusita hata kumuweka benchini katika mechi mbili msimu huu, akimwonyesha kwamba hana nafasi ya kudumu ya kuanza kila mchezo.

Hata hivyo, Mbrazil huyo amepinga hali hiyo na kumfikishia malalamiko yake rais wa klabu Florentino Perez ambaye pia amemweleza Vinicius namna pekee ya kuondokana na suala hilo ni kurejea kwenye kiwango chake cha juu cha zamani.

Wakala wake, Frederico Pena, alifanya kikao Jumatatu na Mkurugenzi Mtendaji pamoja na Makamu wa Rais wa Madrid, Jose Angel Sanchez, kujadili masuala  ya mkataba mpya.

Licha ya kwamba  bado amebakiza misimu miwili kwenye mkataba wake wa sasa, mazungumzo hayo hayajapata mwafaka.

Awali, pande zote zilikuwa karibu kufikia makubaliano ya kumuongeza mkataba mpya miezi sita iliyopita. Hata hivyo, madai ya nyongeza ya mshahara kutoka kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 yalisababisha klabu kusitisha mazungumzo hayo wakati wa Kombe la Dunia la Klabu, na wakala wake ameambiwa wazi kuwa hawatampa ofa zaidi ya hiyo iliyotolewa.

Vinicius aliwahi kuhusishwa na dili kubwa la kutua Saudi Arabia mwaka 2024, lakini alisisitiza kuwa anataka kubaki Madrid.

 Hata hivyo, ikiwa hakutakuwa na makubaliano mapya kuna uwezekano Vini akaomba kuondoka na kutua kwa matajiri hao wa Saudi Arabia.

Hadi sasa, Vinicius amefunga mabao mawili na kutoa pasi mbili za mabao katika La Liga.