Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vinicius Jr ashinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia Fifa

Muktasari:

  • Vinicius Jr, ambaye alifanikiwa kushinda tuzo hiyo kwa pointi 48 dhidi ya 43 za Rodri na 37 za Jude Bellingham, alizua mjadala mkubwa Oktoba mwaka huu alipokosa tuzo ya Ballon d'Or mbele ya Rodri ambaye hakuwa anapewa nafasi kama yeye.

DOHA, QATAR: BAADA ya kukosa tuzo ya Ballond d'Or mbele ya Rodri, staa wa Real Madrid na Brazil, Vinicius Jr ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa FIFA wa mwaka katika sherehe zilizofanyika  jana huko Doha, Qatar.

Vinicius Jr, ambaye alifanikiwa kushinda tuzo hiyo kwa pointi 48 dhidi ya 43 za Rodri na 37 za Jude Bellingham, alizua mjadala mkubwa Oktoba mwaka huu alipokosa tuzo ya Ballon d'Or mbele ya Rodri ambaye hakuwa anapewa nafasi kama yeye.

Tuzo hii ya FIFA imezingatia kuchagua wachezaji waliopata mafanikio kuanzia Agosti mwaka jana hadi Agosti mwaka huu ambao hutangazwa kisha hupigiwa kura.

Katika kipindi hicho Vinicus ameshinda mataji matano akiwa na Real Madrid  na yeye akiwa ndio mchezaji muhimuo katika kikosi pamoja na Jude Bellingham.

Mbali ya Vinicius kwa upande wa kipa bora, Emiliano Martinez wa Aston Villa, ambaye aliwahi kushinda tuzo hii mwaka 2022, alichaguliwa tena kipa bora ukiwa ni mwaka wa mafanikio zaidi kwake kwani alishinda pia tuzo ya kipa bora katika tuzo za Ballon d'Or 2024.

Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti ndio alichaguliwa kuwa kocha bora wa mwaka wa FIFA kutokana na mafanikio makubwa aliyopata akiwa na Madrid, akichukua mataji matano kuanzia Agosti mwaka jana.

Kwa upande wa wanawake, kiungo wa Barcelona ambaye ni raia wa Hispania, Aitana Bonmati alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka, huku Alyssa Naeher wa Chicago Red Stars  akanyakuwa tuzo ya kipa bora.

Kocha bora kwa upande wa wanawake aliibuka Emma Hayes aliichukua tuzo hiyo kwa mafanikio yake akiwa na Chelsea ambayo aliipa ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake England kwa msimu uliopita.