Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vichaka vya straika Isak msimu ujao

ISAK pict

Muktasari:

  • Isak alikuwa muhimu kwenye michuano hiyo ya Kombe la Ligi na alifunga mabao matatu, ikiwamo kwenye mechi ya nusu fainali dhidi ya Arsenal na kwenda fainali dhidi ya Liverpool, Jumapili iliyopita.

NEWCASTLE, ENGLAND: NEWCASTLE United itakuwa kwenye presha kubwa ya kupambana kubaki na huduma ya straika wao wa mabao, Alexander Isak dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi hasa baada ya kuwaongoza kushinda taji lao la kwanza katika kipindi cha miaka 70.

Isak alikuwa muhimu kwenye michuano hiyo ya Kombe la Ligi na alifunga mabao matatu, ikiwamo kwenye mechi ya nusu fainali dhidi ya Arsenal na kwenda fainali dhidi ya Liverpool, Jumapili iliyopita.

Straika huyo wa kimataifa wa Sweden amefunga mabao 23 kwenye michuano yote msimu huu akiwa na kikosi cha Newcastle. Kiwango chake cha uwanjani kinamfanya awe kwenye rada za timu nyingi zinazohitaji huduma yake dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Je, ni wapi Isak anapaswa kwenda kukipiga msimu ujao kuendelea kutamba uwanjani?

ISA 01

Arsenal

Haya yanaweza kuwa makazi yajayo ya Isak. Uhamisho wa kwenda Emirates umekuwa ukipigiwa kelele na mashabiki na wachambuzi wakiambia Arsenal mchezaji Namba 9, ambaye anafaa kwenda kwenye kikosi chao. Isak amefunga mara mbili dhidi ya Arsenal msimu huu, mara ya kwanza kwenye ushindi wa 1-0 uwanjani St James' Park na pili kwenye ushindi wa 2-0 huko Emirates, huku mechi zote hizo ilizopoteza Arsenal ilitokana na kushindwa kuwa na watu sahihi kwenye fowadi yao. Kutokana na hilo, Kocha Mikel Arteta anahitaji straika mpya dirisha lijalo huku Isak anaweza kuwa chaguo sahihi.

ISA 02

Liverpool

Kama Liverpool itaingia kwenye vita ya kumsaka Isak, basi watakaokuwa kwenye matatizo makubwa ni Arsenal. Liverpool wapo kwenye nafasi nzuri ya kushinda ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu na hilo linaweza kuwa kishawishi cha kwenda kumnasa Isak, hasa ikitambua kuna wachezaji wataondoka kwenye kikosi chao wakati dirisha lijalo litakapofunguliwa. Supastaa Mohamed Salah mkataba wake unafika tamati mwisho wa msimu, hivyo kama hatabaki Liverpool inaweza kumchagua Isak kwenye kuziba pengo lake huko Anfield baada ya Darwin Nunez na Luis Diaz nao kuhusishwa na mpango wa kuondoka.

ISA 03

Real Madrid

Isak ameonyesha kiwango bora sana kiasi cha kuifanya klabu yoyote ile kuhitaji saini yake na Real Madrid ni miongoni mwa timu zinazopiga hesabu ya kwenda kumnasa straika huyo. Staa huyo wa Sweden alishawahi kucheza kwenye La Liga, wakati alipoitumikia Real Sociedad kwa misimu kadhaa na kufunga mabao 44 katika mechi 132, ikiwamo kufunga mabao 17 katika msimu mmoja wa La Liga, aliocheza mechi 34, hivyo Madrid inafahamu mchezaji wanayemtaka, atakwenda kuwapa kitu uwanjani, hasa baada ya kufunga mabao 48 katika misimu yake miwili ya mwisho aliyocheza England. Isak akitua, Madrid itatisha.

ISA 05

Barcelona

Chaguo jingine bora kwa Isak kwenye kuboresha kiwango chake ni kwenda kukipiga Nou Camp baada ya kuripotiwa skauti wa Barcelona walikwenda kumtazama mshambuliaji huyo kwenye mechi ya ushindi wa bao 1-0 iliyopata Newcastle dhidi ya West Ham. Bosi wa Barcelona, Joan Laporta ni shabiki mkubwa wa Isak na hilo linampa nafasi kubwa ya mshambuliaji huyo kunaswa hasa kipindi hiki ambacho anasakwa mtu wa kuja kuchukua mikoba ya Robert Lewandowski, atakayetimiza umri wa miaka 37 kwenye dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Barca inamtazama Isak kama mtu sahihi kwenye hilo.

ISA 04

Kubaki Newcastle

Kuna stori nyingi zinazomhusisha Isak na mpango wa kuachana na miamba hiyo ya St James' Park, lakini hakuna ubaya pia kama atabaki kwenye timu hiyo. Newcastle ni mahali ambako Isak amejitengeneza na kuwa gumzo kubwa, hivyo ataendelea kuwa matata endapo atabaki kwenye kikosi hicho. Amesaidia timu hiyo kubeba mataji lao la kwanza tangu mwaka 1955 na timu ipo kwenye wakati mzuri wa kukamatia tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya, jambo ambalo linaweza kumshawishi mshambuliaji huyo akaamua kubaki kwenye kikosi hicho na kuendelea kufurahia mafanikio yake. Kubaki ni chaguo jingine sahihi kwa Isak.