Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Van Persie atimuliwa Feyenoord

VAN P Pict

Muktasari:

  • Van Persie, ambaye ni mmoja wa magwiji wa soka la nchi hiyo, aliiongoza Feyenoord kumaliza nafasi ya pili katika Eredivisie msimu uliopita na kufuzu moja kwa moja kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini viongozi wa klabu wameona ni wakati wa kuanza ukurasa mpya.

ROTTERDAM, UHOLANZI: FEYENOORD imeachana rasmi na kocha wake, Robin van Persie baada ya miezi 16 pekee ya kuitumikia timu hiyo, uamuzi ambao umezua mjadala mkubwa ndani na nje ya soka la Uholanzi.

Van Persie, ambaye ni mmoja wa magwiji wa soka la nchi hiyo, aliiongoza Feyenoord kumaliza nafasi ya pili katika Eredivisie msimu uliopita na kufuzu moja kwa moja kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini viongozi wa klabu wameona ni wakati wa kuanza ukurasa mpya.

Kocha huyo mwenye miaka 42 anaondoka wiki mbili tu baada ya Devy Rigaux kuteuliwa kuwa mkurugenzi wa ufundi huku Robert Eenhoorn akichukua nafasi ya meneja mkuu wa klabu.

VAN 02

Rigaux amesema licha ya mafanikio ya kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya, tathmini ya ndani imeonyesha timu imeanza kupungua kiwango katika maeneo kadhaa muhimu.

“Robin van Persie ametoa kila kitu kwa ajili ya klabu katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu,” amesema Rigaux.

“Anastahili pongezi kwa namna alivyoiongoza timu kumaliza nafasi ya pili katika msimu mgumu na kutupa nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.”

Aliendelea: “Tulifanya uchambuzi wa kina wa ndani. Tulitazama maendeleo ya mfumo wa uchezaji pamoja na mwenendo wa kupungua kwa pointi katika mashindano ya ndani na Ulaya.

“Hitimisho letu ni kwamba ni bora kuanza msimu mpya chini ya kocha mpya.”

Van Persie ni miongoni mwa wachezaji wanaoheshimika zaidi katika historia ya Feyenoord. Alianza soka lake la kulipwa hapo kabla ya kurejea mwishoni mwa maisha yake ya soka.

Katika vipindi vyake viwili akiwa mchezaji wa Feyenoord, alifunga mabao 46 katika mechi 122.

VAN 01

Baada ya kustaafu, alifanya kazi ya ukocha katika timu za vijana kabla ya kuwa msaidizi wa Dick Advocaat.

Mwaka 2024 alikwenda kuinoa Heerenveen lakini akarudi Feyenoord miezi tisa baadaye na kupewa jukumu la kuwa kocha mkuu.

Mbali na Feyenoord, Van Persie alijijengea jina kubwa akiwa Arsenal ambako alicheza kwa miaka minane na kushinda Kombe la FA kabla ya kuhamia Manchester United mwaka 2012.

Katika msimu wake wa kwanza Old Trafford aliisaidia United kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England, mafanikio ambayo yaliimarisha hadhi yake kama mmoja wa washambuliaji bora kuwahi kutokea Ulaya.

Mashabiki sasa wanasubiri kuona nani atachukua nafasi yake kwa ajili ya msimu mpya.