Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Van Dijk, Mo Salah waangushiwa jumba Liverpool

LIVERPOOL Pict

Muktasari:

  • Liverpool ilinyakua ubingwa wa Ligi Kuu England msimu uliopita na Slot ilikuwa mwaka wake wa kwanza kwenye kikosi hicho kabla ya kusajili mastaa kibao dirisha lililopita.

LIVERPOOL, ENGLAND: WAYNE Rooney amesema mastaa wawili wa Liverpool, Virgil van Dijk na Mohamed Salah wanapaswa kupambana kwa nguvu zao kumsaidia Kocha Arne Slot.

Liverpool ilinyakua ubingwa wa Ligi Kuu England msimu uliopita na Slot ilikuwa mwaka wake wa kwanza kwenye kikosi hicho kabla ya kusajili mastaa kibao dirisha lililopita.

Lakini, kiwango chao kimeangukia pua msimu huu. Na sasa ipo nyuma kwa pointi saba kwa vinara wa ligi, Arsenal baada ya kukumbana na vichapo vinne mfululizo.

Slot mambo yake yalikuwa safi msimu uliopita, lakini safari hii yupo kwenye wakati mgumu kwelikweli, anawaza juu ya usalama wa kibarua chake huko Anfield.

Na Rooney anadhani Van Dijk na Mo Salah wanamwangusha kocha wao, Slot.

Kwenye kipindi cha The Wayne Rooney Show, amesema: “Kipindi hiki kocha na wachezaji viongozi kwenye timu wanapaswa kutafuta suluhu haraka. Virgil van Dijk na Mohamed Salah, walisaini dili mpya, lakini sidhani kama wamefanya kitu kikubwa msimu huu.

LIVER 01

“Nadhani tu lugha ya ishara inakuonyesha mengi, wale ni wachezaji wawili wakubwa na wanapokuwa hawapo vizuri, hilo linamwathiri kila mtu kwenye timu.

“Naweza nisieleweke kwenye hili, lakini kama ningekuwa shabiki wa Liverpool au kocha wao, ningekuwa na wasiwasi mkubwa juu ya jambo hili.”

Ilionekana kama ushindi kwa mabosi wa Liverpool wakati ilipofanikiwa kuwasainisha mikataba mipya Van Dijk na Salah, Aprili mwaka huu. Lakini, ilisahaulika wawili hao wote walikuwa wamefikia kwenye umri wa miaka 30 na sasa viwango vyao vinakaribia kuporomoka.

LIVER 02

Mo Salah amefunga mabao manne katika mechi 13 alizocheza katika michuano yote msimu huu na kiwango chake kimeshuka, huku Van Dijk akipoteza hadhi yake ya kuwa beki bora kwenye Ligi Kuu England msimu huu.

Liverpool ina kazi ya kuweka mambo sawa, kwanza kwenye mechi ya Kombe la Ligi dhidi ya Crystal Palace itakayopigwa Jumatano, kabla ya kuwa na mechi tatu ngumu zaidi, dhidi ya Aston Villa, Real Madrid na Manchester City.