Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Carragher: Liverpool? Haya ni majanga

LIVERPOOL Pict

Muktasari:

  • Mwanzo mzuri wa Liverpool kwenye Ligi Kuu England umekumbana na kisiki kwa siku za karibuni kutokana na kupoteza mfululizo na hivyo kuachwa nyuma kwa pointi saba na Arsenal.

LIVERPOOL, ENGLAND: BEKI wa zamani wa Liverpool, Jamie Carragher amekiri klabu yake hiyo ya zamani ipo kwenye kipindi kigumu baada ya kupoteza mechi nne mfululizo Ligi Kuu England na hivyo kuachwa pointi kibao na Arsenal iliyoko kileleni kwenye msimamo.

Mwanzo mzuri wa Liverpool kwenye Ligi Kuu England umekumbana na kisiki kwa siku za karibuni kutokana na kupoteza mfululizo na hivyo kuachwa nyuma kwa pointi saba na Arsenal.

Kikosi hicho cha Kocha Arne Slot kilianza kwa kupoteza mbele ya Crystal Palace na Chelsea kabla ya mapumziko ya kupisha mechi za kimataifa.

LIVER 01

Ligi iliporejea, ilijikuta ikipoteza mara nyingine mbili mfululizo dhidi ya Manchester United uwanjani Anfield na Brentford ugenini na hivyo kuifanya timu hiyo kuandika rekodi mbaya.

Liverpool imeonyesha udhaifu mkubwa wa kukabiliana na pasi za mipira mirefu, hasa ile inayopigwa kwenye boksi lao na wapinzani wametumia hilo kama fimbo ya kuwaadhibu.

Carragher amesema: “Kupoteza mechi nne mfululizo ni janga. Kuona mabingwa na tena waliofanya matumizi makubwa kwenye usajili wanakuwa kwenye hali hiyo, hilo ni tatizo.

SLOT Pict

“Lazima kutakuwa na maswali mengi sana ya kuulizana kwenye vyumba vya kubadilishia kati ya wachezaji na makocha. Ukitazama namna ilivyotumia pesa kusajili, unaona kabisa LIverpool inahitaji mambo mazuri zaidi na zaidi. Liverpool inaonekana kuwa na wachezaji warefu na wenye nguvu, lakini wanachokifanya, hakitoshi.”

Liverpool iliuza baadhi ya mastaa wake kwenye dirisha lililopita la majira ya kiangazi akiwamo Trent Alexander-Arnold, Luis Diaz na Darwin Nunez na ilitumia zaidi ya Pauni 400 milioni kunasa huduma za mastaa wengine kama Hugo Ekitike, Alexander Isak, Florian Wirtz na Jeremie Frimpong kuja kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho.

SLO 01

Lakini, sasa kikosi hicho cha kocha Slot kimekuwa na udhaifu mkubwa kwenye safu yake ya ulinzi na hadi sasa kimesharuhusu mabao 14 na hivyo kutishia uwezekano wao wa kutetea taji la Ligi Kuu England msimu huu.