Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Liverpool inavyoelekea katika rekodi mbaya za mabingwa watetezi

LIVERPOOL Pict

Muktasari:

  • Miamba hiyo ya Anfield ilifanya usajili wa nguvu, wakiongeza wachezaji wapya kila upande wa uwanja, ingawa pengine kusajili mabeki zaidi kungekuwa wazo bora. Kila kitu kilianza vizuri, kwa ushindi katika mechi tano za kwanza.

LONDON, ENGLAND: MAISHA yanakwenda kasi sana. Baada ya msimu uliopita kutawala kwa urahisi wa kushangaza, Liverpool ilionekana kuwa tayari kutetea taji lao la Ligi Kuu England kwa nguvu zote katika msimu wa 2025/26.

Miamba hiyo ya Anfield ilifanya usajili wa nguvu, wakiongeza wachezaji wapya kila upande wa uwanja, ingawa pengine kusajili mabeki zaidi kungekuwa wazo bora. Kila kitu kilianza vizuri, kwa ushindi katika mechi tano za kwanza.

Lakini ghafla, mambo yamekwenda kombo. Liverpool imepoteza mechi nne mfululizo za ligi na kupoteza uongozi wao wa pointi tano kimegeuka kuwa pengo la pointi saba dhidi ya viongozi wa ligi.

Arsenal wamewapita, lakini si wao pekee kuna Bournemouth, Tottenham, Sunderland, Manchester City, na hata Manchester United sasa wako juu yao. Kwa klabu yenye hadhi ya Liverpool, hili ni pigo kubwa.

Kile kilichoonekana changamoto ndogo sasa kimekuwa mgogoro mkubwa. Na hata kama kocha Arne Slot ataweza kurejea katika ubora wake, nafasi ya kulinda taji lao tayari inaonekana imetoweka.

Hali hii imewafanya wachambuzi wa soka waanze kujiuliza, je, Liverpool wanajiandaa kuingia katika orodha ya mabingwa watetezi 10 waliowahi kufanya vibaya na kushindwa kubeba taji la ligi?

Hizi ndizo timu ambazo, baada ya utukufu wa kushinda taji, zilianguka vibaya katika msimu uliofuata.

LIVER 10

10. Arsenal (2004/05)

Baada ya kutwaa ubingwa wa 2003/04 bila kupoteza mchezo wowote, Arsenal iliingia msimu uliofuata ikiwa na majivuno ya “The Invincibles”. Lakini ilishindwa kurudia maajabu hayo, ikipoteza mechi tano na kumaliza na pointi 12 nyuma ya Chelsea ya Jose Mourinho.

Kipigo chao cha kwanza kilitokea Old Trafford dhidi ya Man United, matokeo yaliyozua utata mkubwa na yaliyovunja kabisa hali yao ya kutokushindwa. Tangu hapo, ilipoteza nguvu na haijawahi kushinda taji la ligi tena.

LIVER 09

9. Man United (2001/02)

Baada ya miaka ya mafanikio chini ya Sir Alex Ferguson, Manchester United ilishuka ghafla hadi nafasi ya tatu msimu wa 2001/02, jambo lililokuwa gumu kuamini kwa mashabiki wao.

Wakiwa na vipigo vitano katika kipindi cha mechi saba, walijikuta wakipoteza uelekeo, wakimaliza msimu bila taji lolote. Zaidi ya hayo, Arsenal waliwapora ubingwa kwa ushindi wa 1–0 katika Uwanja wa Old Trafford, fedheha kwa kocha na klabu.

LIVER 08

8. Chelsea (2017/18)

Antonio Conte aliingia England kwa kishindo msimu wa 2016/17, akishinda taji katika msimu wake wa kwanza. Lakini mafanikio hayo hayakudumu.

Msimu uliofuata wachezaji wake walionekana kuchoka na mfumo wa mabeki watatu, huku Conte akionekana kukasirika kwa kukosa usajili aliotaka. Matokeo yakawa mabaya, walishuka hadi nafasi ya tano, ingawa walipata faraja kwa kutwaa Kombe la FA. Ilikuwa ishara nyingine ya tabia ya Chelsea ya kupanda na kushuka kwa kasi kubwa.

LIVER 07

7. Blackburn Rovers (1995/96)

Mwaka 1995, Blackburn Rovers ilishangaza dunia kwa kutwaa ubingwa chini ya Kocha Kenny Dalglish, wakiongozwa na washambuliaji Alan Shearer na Chris Sutton.

Lakini baada ya Dalglish kuondoka, timu iliporomoka haraka. Wakamaliza nafasi ya saba, wakitolewa mapema katika mashindano ya Kombe la FA na wakafanya vibaya kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya. Ushawishi wao ukaisha papo hapo.

LIVER 06

6. Liverpool (2020/21)

Baada ya miaka 30 bila taji, Liverpool ilishinda ubingwa wa Ligi Kuu England 2019/20 kwa pointi 99, na kila mtu aliamini wamefufuka.

Lakini msimu uliofuata ukawa wa maumivu. Walipoteza mechi sita za nyumbani mfululizo, rekodi mbaya zaidi katika historia ya klabu. Majeruhi ya wachezaji muhimu kama Van Dijk na Gomez yaliharibu safu ya ulinzi. Hata hivyo, walipambana kurejea na kumaliza nafasi ya tatu, wakinusurika aibu kubwa zaidi.

LIVER 05

5. Man City (2024/25)

Kuweka Manchester City hapa juu inaonekana kali, lakini kiwango walichokuwa wamezoea kinakataa visingizio. Baada ya kutwaa mataji manne mfululizo, timu ya Pep Guardiola ilionekana haina mpinzani.

Kisha ghafla, ikapoteza mwelekeo. Kati ya Oktoba na Desemba 2024, ilicheza mechi 13 katika mashindano yote na kushinda moja pekee.

Walishindwa na Bournemouth, Brighton, Sporting Lisbon, na mara mbili mbele ya Tottenham.

Man City ilimaliza nafasi ya tatu, ikiwa mbali na ubingwa na msimu ukawa wa kukatisha tamaa.

LIVER 04

4. Man United (2013/14)

Baada ya Sir Alex Ferguson kustaafu, David Moyes alirithi kiti kigumu zaidi England.

Ndoto ikawa ndoto mbaya. Man United ilimaliza nafasi ya saba, ikiwa na pointi 25 pungufu kuliko msimu uliopita.

Walishindwa mara sita nyumbani, wakapoteza makombe yote na wakashindwa kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza tangu 1995.

Ukosefu wa usajili sahihi, badala ya kuwasajili Gareth Bale, Toni Kroos na Cesc Fabregas wakamnasa Marouane Fellain na kuonyesha wazi pengo kubwa lililoachwa na Ferguson.

LIVER 03

3. Chelsea (2015/16)

Baada ya mafanikio ya 2014/15, Jose Mourinho alirudi kwa tabia yake ya tatu ya “kujiharibia”.

Msimu ulianza vibaya pale alipomkosoa daktari wa timu hadharani, hali iliyochafua hewa ndani ya klabu. Kufikia Desemba, Chelsea ilikuwa pointi moja tu juu ya mstari wa kushuka daraja.

Mourinho akafutwa kazi, Guus Hiddink akaokoa jahazi na kumaliza ligi katikati ya msimamo. Lakini kushuka kwa pointi 37 kulilinganishwa na mwaka uliopita na ilikuwa ni aibu.

LIVER 02

2. Leicester City (2016/17)

Leicester City iliingia msimu wa 2016/17 wakiwa mashujaa wa dunia. Lakini hali ikabadilika haraka. Wakawauza baadhi ya mastaa wao akiwamo N’Golo Kanté na kusababisha kupata matokeo mabovu.

Hadi kufikia Februari ilikuwa pointi moja tu juu ya mstari wa kushuka daraja na Kocha Claudio Ranieri akafutwa kazi na Craig Shakespeare kuchukua mikoba akiisaidia kumaliza nafasi ya 12. Ulikuwa mwanzo wa mwisho wa hadithi yao ya kisanii.

LIVER 01

1. Leeds United (1992/93)

Leeds United ilikuwa mabingwa wa mwisho wa Ligi ya Daraja la Kwanza kabla ya kuzaliwa kwa Ligi Kuu England. Lakini, msimu uliofuata ukawa wa aibu kubwa, hawakushinda hata mechi moja ugenini, wakamaliza nafasi ya 17 kati ya timu 22, pointi mbili tu juu ya kushuka daraja.

Walipoteza ubora wao wote na hata mashindano ya Ulaya hayakuwasaidia. Huu ndio ulikuwa wakati mbaya zaidi wa bingwa mtetezi kuboronga kwenye mchakamchaka wa kutetea taji msimu uliofuata.