Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Uruguay kimeumana huko

URUGUAY Pict

Muktasari:

  • Uruguay 'La Celeste' ilikuwa ni moja ya timu iliyopewa nafasi ya kufanya vizuri katika fainali za Kombe la Dunia, mambo yalibadilika na kujikuta wakiondolewa mapema mashindanoni, baada ya kumaliza katika nafasi ya tatu ya Kundi H nyuma ya vinara Hispania na timu ndogo ya Cape Verde.

MIAMI, MAREKANI: WACHEZAJI wa timu ya taifa ya Uruguay wamepata pigo jingine baada Shirikisho la Soka la Uruguay (AUF) kuchukua uamuzi kuvunja kambi na kila mtu kutakiwa kujigharamia mwenyewe safari ya kuwarudisha nyumbani.

Uruguay 'La Celeste' ilikuwa ni moja ya timu iliyopewa nafasi ya kufanya vizuri katika fainali za Kombe la Dunia, mambo yalibadilika na kujikuta wakiondolewa mapema mashindanoni, baada ya kumaliza katika nafasi ya tatu ya Kundi H nyuma ya vinara Hispania na timu ndogo ya Cape Verde.

Kikosi cha kocha Marcelo Bielsa kilithibitisha kuondolewa kwake baada ya kufungwa bao 1-0 na Hispania siku ya Ijumaa, kufuatia sare mbili dhidi ya Cape Verde na Saudi Arabia ambao walimaliza mkiani mwa kundi.

URU 02

Kwa mujibu wa ripoti kutoka Uruguay, AUF ilifuta safari maalumu ya ndege iliyokuwa iwapeleke wachezaji na benchi la ufundi nyumbani kutoka Mexico.

Kutokana na uamuzi huo, kila mchezaji na mwanachama wa benchi la ufundi alilazimika kujigharamia na kupanga safari yake mwenyewe kwa kutumia ndege za kawaida za abiria.

Uruguay, mabingwa wa dunia mara mbili, walikuwa timu ya kwanza kutoka Amerika Kusini kuondolewa katika Kombe la Dunia la mwaka huu.

Hii ni mara ya tatu kwa Uruguay kuishia kuondolewa kwenye hatua ya makundi bila kupata ushindi hata mmoja, baada ya kufanya hivyo pia katika Kombe la Dunia la mwaka 1974 na 1986.

Aidha, walilinganisha rekodi ya Bolivia ya kuwa timu ya Amerika Kusini iliyotolewa kwenye hatua ya makundi bila kushinda hata mchezo mmoja.

URU 01

Kwa upande mwingine, Cape Verde, kwa upande wake, imeandika historia kwa kuwa taifa lenye eneo dogo zaidi kuwahi kufuzu hatua ya mtoano ya Kombe la Dunia.

Kikosi cha kocha Bubista sasa kitakutana na mabingwa watetezi wa dunia, Argentina.

Pia, kipigo cha Uruguay dhidi ya Hispania kilihakikisha rasmi kuwa England imefuzu kwenda hatua ya mtoano ya Kombe la Dunia.