Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Umemuelewa Paul Labile Pogba?

POGBA Pict

Muktasari:

  • BAADHI ya vitabu vya dini vimesema kulipa kisasi ni haki, wahenga wakasema adui unayemuweza usimuachie Mungu, wanafalsafa wakasema msamaha ni kisasi tosha -- ilimradi tu kila mtu amesema lake kuhusu kisasi.

BAADHI ya vitabu vya dini vimesema kulipa kisasi ni haki, wahenga wakasema adui unayemuweza usimuachie Mungu, wanafalsafa wakasema msamaha ni kisasi tosha -- ilimradi tu kila mtu amesema lake kuhusu kisasi.

Juzi kati, mshkaji wetu, Paul Pogba alitukumbusha wimbo wa ‘Kilio cha Mtu Mzima’ wa bendi ya Msondo Ngoma wakati huo ikiitwa OTTU Jazz Band.

Video zilizosambaa katika mitandao ya kijamii zilimuonyesha Pogba akimwaga machozi wakati anasaini mkataba wa miaka miwili wa kuichezea AS Monaco.

Inawezekana ikawa mwanzo wa dunia mpya ya Pogba au ikawa mwendelezo wa dunia yake ya zamani. Yote yanawezekana.

Hadi sasa ana umri wa miaka 32. Baada ya kuachiliwa huru kutoka kifungo chake alichokipata kutokana na kukutwa na hatia ya kutumia dawa zinazopigwa marufuku michezoni, Februari mwaka huu kulikuwa na ofa nyingi mezani zilizoripotiwa kuwa amezipata.

POG 02

Mara kadhaa alionekana Marekani, ilielezwa kwamba alikuwa katika mazungumzo na Inter Miami, baadhi ya timu za Saudi Arabia pia zikahusishwa naye. Lakini yeye akaamua kutushangaza kwa kwenda Monaco.

Kwa umri wake pengine ungetegemea angeangalia zaidi pesa kwa kwenda zake Saudia ambako kuna mavuno makubwa ukizingatia wakati amefungiwa aliwahi kutamka wazi kuwa hali yake ya kiuchumi haikuwa sawa.

Mbali ya Saudia, Miami pia ilitajwa kuwa tayari kumsajili na kumpa mshahara mkubwa. Kote huko amekataa. Ripoti zinaonyesha kwamba Monaco, itakuwa ikimpa mshahara wa Euro 350,000 kwa mwezi.

Kiasi ambacho kwa wiki ni Euro 87,500, pesa ambayo ni kama bonasi kule Saudia.

POG 01
POG 01

Lakini hii ndio njia ambayo ameichagua Pogba, moja kati ya sababu zilizomfanya achague Monaco na sio timu nyingine kwanza ni ushiriki wao wa Ligi ya Mabingwa. Kiungo huyu anaamini bado ana nafasi ya kuwaonyesha kuwa miguu yake bado haijamsaliti.

Ikiwa angechagua njia ya kwenda Marekani au Saudia, pengine ndio ingekuwa mwisho wa maisha yake ya soka, lakini hilo haliingii akili mwake.

Hiki ni kisasi chake Pogba dhidi ya mpira wa Ulaya. Wakati anaondoka Man United kurejea Juventus katika mahojiano yake aliyofanya alisema ‘Man United itaona na itajutia’ kumpoteza, aliamini maisha yake katika kikosi cha Juventus yangeenda kuwa sawa na nyakati zile Pirlo anamuokota, mambo yakawa tofauti. Sio tu hakuwa na kiwango alichotarajia hata kucheza hakuwa anacheza.

POG 03

Kisasi cha Pogba hakikulipwa kwa wakati ule. Kila alipoweka nyayo zake katika ardhi ya Allianz Stadium, miguu ilikuwa ikishindwa kufanya vile ilivyozoea.

Majeraha yalikuwa kama sehemu ya kunywa maji ya kunywa kwake. Mimi na wewe hatujui kama hili litaendelea au ameliacha pale pale kwenye ardhi ya Sergio Mattarella.

Kurudi kwake Monaco ambayo inamhakikishia pia kucheza Ligi ya Mabingwa kwake ndio nafasi pekee ya kulipa kisasi aliyokuwa nayo. Kwanza atapata nafasi ya kucheza moja kati ya ligi tano bora barani Ulaya, pia atacheza michuano ya kimataifa. Huwezi jua matumaini ni kwamba ikiwa atawaka na kuonyesha kiwango bora atakuwepo pia katika kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa, yote yanawezekana.

Swali gumu ni je, kisasi chake kitafanikiwa au kitafeli? Na kama kitafeli nani atakuwa amepoteza kati yake na wale ambao pengine anawahitaji kuwalipia kisasi?

Kisasi cha Pogba si tu dhidi ya wale aliowaapizia, bali ni dhidi ya soka na dunia kwa ujumla. Yeye anataka kuwaonyesha kuwa ni miongoni mwa viungo bora kuwahi kutokea.

Kisasi kama hiki nimewahi kuona mara nyingi. Niliwahi kuona kwa Jose Mourinho kama kocha, baada ya kukataliwa pale Barcelona na nafasi yake akapewa Pep Guardiola, Mourinho aliondoka kwenda kujitafuta akapita sehemu mbalimbali kama FC Porto na baadaye Chelsea, alirejea Nou Camp msimu wa 2009/10 kama kocha akiwa na Inter Milan katika mchezo wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Inter ilipoteza 1-0 lakini ilipita kwa matokeo ya jumla ya 3-1. Baada ya mechi Mourinho alikimbia uwanja mzima akionyesha kidole kimoja kuashiria kuwa yeye ndiye ‘Special One’ na hakuna mwingine.

POG 04

Niliwahi pia kushuhudia kwa Emmanuel Adebayor. Usajili wake wa kujiunga na Manchester City akitokea Arsenal mwaka 2009 ulitikisa sana, mashabiki wa Arsenal walimwita msaliti.

Katika mahojiano aliyofanya kuelezea nyuma ya pazia juu ya kilichotokea, Adebayor anasema wakati aliporejea katika timu kwa ajili ya kuanza maandalizi ya msimu mpya, kocha Arsene Wenger aliamwambia kwamba hahitajiki katika timu.

Siku moja baada ya kuambiwa hivyo, kesho yake alipokwenda mazoezini akaambiwa na mlinzi kwamba haruhusiwi kuingia. Hakuwa na namna ilipokuja ofa ya Man City aliikubali.

Mechi ya nne ya msimu wake wa kwanza akiwa na Man City ambao ulikuwa ni 2009/10 ilikuwa dhidi ya Arsenal, wakati anaingia kiwanjani alisikia mashabiki wa Arsenal waliokuwapo kwenye dimba la Etihad wanaimba wimbo waliokuwa wanamwimbia wakati anacheza katika timu yao lakini wakati huu ilikuwa ni tofauti walikuwa wakitukana wazazi wake.

Vilevile alipoenda kuwasalimia wachezaji wa Arsenal waliokuwa marafiki zake wakati anaichezea timu hiyo, pia wakamkataa, hawakutaka ushkaji naye.

Baada ya hapo akajipiza kwamba lazima awaonyeshe. Kweli akafunga bao la tatu katika mchezo kwa kichwa na akaenda kushangilia katika jukwaa la mashabiki wa Arsenal na akawa amelipa kisasi chake.

Hatujui kwa Pogba itakuwaje, je kisasi atakifanikisha au ataendeleza gundu lake linalomwandama tangu aachane na Man United, ngoja tuone, chozi la kilio cha mtu mzima.