Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Umeme wazua moto nyumbani kwa Vini Junior

UMEME Pict

Muktasari:

  • Staa wa Kibrazili, Vini Jr hakuwapo nyumbani akiwa kwenye majukumu ya timu yake ya taifa ya Brazil wakati nyumba yake inaripotiwa kuungua.

MADRID, HISPANIA: TATIZO la umeme kutoka kwenye chumba cha sauna ndicho kilichoripotiwa kusababisha moto kwenye nyumba ya supastaa wa Real Madrid, Vinicius Jr.

Staa wa Kibrazili, Vini Jr hakuwapo nyumbani akiwa kwenye majukumu ya timu yake ya taifa ya Brazil wakati nyumba yake inaripotiwa kuungua.

Mamlaka za usalama za Hispania ziliitwa huko La Moraleja, kaskazini mwa Madrid katika mji wa Alcobendas. Zimamoto walikimbilia eneo la tukio asubuhi ya saa tano, Alhamisi kwenda kupambana na moto huo kwenye nyumba ya Vinicius Jr na kufanikiwa kuuzima saa moja baadaye. Kinachoelezwa ni kwamba kulikuwa na tatizo la kiufundi la umeme kwenye chumba cha sauna na ndiko ulikoanzia moto huo.

UME 02
UME 02

Kwa mujibu wa gazeti la AS la Hispania, chumba cha sauna kimeharibiwa vibaya na moto huo. Na kwamba sehemu nyingine za nyumba hiyo ziliathirika kwa moshi tu.

Kwa mujibu wa taarifa ya maofisa wa usalama ni kwamba hakuna aliyejeruhiwa au kupata madhara kutokana na kuvuta hewa yenye moshi.

Vini anaamini atakaporejea atakuta mazingira mazuri akitokea kwenye majukumu ya kuitumikia timu yake ya taifa. Brazil ilikuwa na mechi dhidi ya Korea Kusini huko Seoul na Jumanne itakipiga na Japan jijini Tokyo.

UME 01

Mshambuliaji huyo wa Kibrazili amekuwa na maisha mazuri chini ya kocha mpya wa Real Madrid, Xabi Alonso baada ya kufunga mabao matano na kuasisti manne katika mechi nane.

Los Blancos inashika usukani wa La Liga baada ya mechi nane, ikishinda saba na kupoteza moja kwa kipigo kizito cha mabao 5-2 kutoka kwa mahasimu wao Atletico Madrid. Mchezaji mwenzake Vinicius, Kylian Mbappe ndiye anayeongoza kwa mabao kwenye La Liga, akiwa amefunga tisa.