Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ukizungumza kwa kujiziba mdomo uwanjani, nyekundu

NYEKUNDU Pict

Muktasari:

  • Tabia za wachezaji zimekuwa zikichunguzwa zaidi katika wiki za hivi karibuni kufuatia sakata la ubaguzi wa rangi lililomhusisha winga wa Real Madrid, Vinicius Junior na mchezaji wa Benfica, Gianluca Prestianni.

ZURICH, USWISI: RAIS wa FIFA, Gianni Infantino, amefichua kuwa wachezaji wanaweza kutolewa nje kwa kadi nyekundu endapo watainua jezi zao na kufunika midomo wanapozungumza na wachezaji wa timu pinzani.

Tabia za wachezaji zimekuwa zikichunguzwa zaidi katika wiki za hivi karibuni kufuatia sakata la ubaguzi wa rangi lililomhusisha winga wa Real Madrid, Vinicius Junior na mchezaji wa Benfica, Gianluca Prestianni.

Prestianni alituhumiwa kutoa kauli ya kibaguzi kwa Vinicius huku akifunika uso wake. Hata hivyo, amekanusha tuhuma hizo, akidai kuwa badala yake alitoa tusi la ushoga.

UEFA imeanzisha uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo, huku Prestianni akisimamishwa kwa muda wakati uchunguzi ukiendelea. FIFA inaripotiwa kuzingatia adhabu kwa wachezaji wanaofunika midomo yao wanapozungumza uwanjani, jambo ambalo Infantino amethibitisha.

Akizungumza na Sky News, alisema: “Iwapo mchezaji atafunika mdomo wake na kusema jambo ambalo lina matokeo ya kibaguzi, basi anapaswa kutolewa nje, bila shaka. Inapaswa kuwepo dhana kwamba amesema jambo ambalo hakupaswa kusema, la sivyo asingekuwa na sababu ya kufunika mdomo wake. Sielewi kabisa kama huna kitu cha kuficha, kwa nini ufunike mdomo wako unapozungumza?”

Infantino aliongeza: “Hivyo ndivyo ilivyo, rahisi tu. Hizi ni hatua tunazoweza na tunazopaswa kuchukua ili kuonyesha uzito katika mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi.”

Inaripotiwa majadiliano kuhusu sheria hiyo bado yako katika hatua za awali na hakuna utekelezaji wa haraka unaotarajiwa. Hata hivyo, pendekezo hilo linaungwa mkono na vyama vya soka vya England ambavyo ni sehemu ya International Football Association Board (IFAB) pamoja na FIFA, baada ya wazo hilo kupendekezwa katika kikao cha kiufundi wiki hii.

Kocha wa zamani wa Manchester United na sasa kocha wa Benfica, Jose Mourinho, pia alitoa maoni yake kuhusu tukio hilo kati ya Vinicius na Prestianni, akichukua msimamo mkali na kusema: “Kama mchezaji ana hatia, sitamtazama tena usoni na atakuwa amemaliza na mimi, lakini ninahitaji kuweka ‘kama’ nyingi kabla ya hapo. Niko dhidi ya aina zote za ubaguzi na ubaguzi wa rangi. Kama mchezaji wangu hakuheshimu misingi hiyo, ambayo pia ni ya Benfica, basi maisha yake ya soka chini ya kocha anayeitwa Mourinho na katika klabu kama Benfica yatakuwa yamekwisha.”