Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Iran hatarini kushiriki Kombe la Dunia 2026, FIFA yatoa tamko

IRAN Pict

Muktasari:

  • Mvutano kati ya Iran, Marekani, na Israel umeongezeka kwa kasi siku ya Ijumaa na Jumamosi, huku pande zote zikishambuliana kwa mabomu.

NCHI ya Iran huenda ikajiondoa kwenye mashindano ya Kombe la Dunia 2026 kufuatia mashambulizi ya anga ya Marekani yaliyomuua kiongozi mkuu wa nchi hiyo, Ayatollah Ali Khamenei.

Mvutano kati ya Iran, Marekani, na Israel umeongezeka kwa kasi siku ya Ijumaa na Jumamosi, huku pande zote zikishambuliana kwa mabomu.

Katika operesheni ya kijeshi ya pamoja, Rais wa Marekani, Donald Trump na nchi ya Israel walishambulia miji mikuu ya Iran, ikiwemo mji mkuu wa Tehran. Trump aliapa kuwapiga kwa nguvu ambayo haijawahi kuonekana hapo awali.

Serikali ya Iran ililipa kisasi kwa kurusha makombora katika nchi jirani zikiwemo Saudi Arabia na Qatar.

Ndege za kivita za England zililazimika kurushwa ili kulinda mataifa washirika, hali inayomaanisha kuwa mataifa matano yanayoshiriki fainali za Kombe la Dunia yameingia kwenye mgogoro huo.

Kufuatia hali hiyo, Rais wa Shirikisho la Soka la Iran, Mehdi Taj, ameweka shaka kubwa kuhusu ushiriki wa nchi hiyo katika mashindano hayo yatakayofanyika Marekani, Canada, na Mexico baada ya miezi mitatu ijayo.

"Kutokana na kile kilichotokea leo na shambulio hilo la Marekani, ni vigumu kwetu kutazamia kushiriki Kombe la Dunia," Taj amekaririwa na gazeti la Marca.

Hata hivyo, ameongeza kuwa uamuzi wa mwisho utatolewa na viongozi wa michezo nchini humo.

Iran imepangwa katika kundi moja na New Zealand, Ubelgiji, na Misri, huku mechi yao ya kwanza ikipangwa kufanyika Juni 16, 2026 huko Los Angeles na Seattle. 

Ikiwa timu ya taifa hilo itafanya vizuri kwenye mashindano hayo inaweza kukutana na Marekani katika hatua ya 32 bora mnamo Julai 3, 2026 huko Dallas.

Licha ya hali hiyo, Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) limeeleza matumaini kuwa mashambulizi hayo hayataathiri mashindano hayo. 

Katibu Mkuu wa FIFA, Mattias Grafstrom, amesema: "Tunaendelea kufuatilia kwa karibu yanayojiri. Lengo letu ni kuwa na Kombe la Dunia salama ambalo kila mshiriki atakuwepo."

Hata kama hali hiyo itatulia, mashabiki wa Iran wanakabiliwa na changamoto ya kukosa viza za kuingia Marekani kwani nchi hiyo tayari ipo kwenye orodha ya mataifa yaliyozuiliwa kuingia Marekani.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu wa England, Keir Starmer, amelaani mashambulizi ya Iran dhidi ya nchi jirani na kutoa wito kwa uongozi wa Iran kutafuta suluhu ya mazungumzo, huku akisisitiza kuwa ndege za England zilitumika tu kwa ajili ya ulinzi na si kushambulia.