Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ujumbe wa dakika 15 wa Tuchel waibeba England Kombe la Dunia

Muktasari:

  • England walijikuta wakivunjika moyo baada ya kuruhusu bao la kusawazishwa kwa mara ya pili ndani ya dakika 45 za kwanza, licha ya kuwa walikuwa wameongoza mchezo.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa England, Thomas Tuchel amefichua alichowaambia wachezaji wake wakati wa mapumziko ya kipindi cha kwanza katika mchezo wa ufunguzi wa Kombe la Dunia, huku akisisitiza kuwa utulivu na kujiamini ndivyo vilivyobadili sura ya mechi hiyo.

England walijikuta wakivunjika moyo baada ya kuruhusu bao la kusawazishwa kwa mara ya pili ndani ya dakika 45 za kwanza, licha ya kuwa walikuwa wameongoza mchezo. Hata hivyo, Tuchel hakuchagua kukasirika wala kutoa maagizo ya haraka. Badala yake, aliwataka wachezaji wake watulie na kujikusanya upya.

"Niliketi pamoja nao na kuwapa muda wa kutulia. Nilikuwaambia wapunguze presha kwa sababu tulikuwa tumefungwa bao tu. Nilihitaji watulize hisia zao kabla ya kuendelea kucheza kwa mtindo wetu," alisema Tuchel.

Mjerumani huyo alieleza kuwa hakuruhusu matokeo ya muda huo kubadilisha mtazamo wake kuhusu kikosi chake, hasa baada ya siku 17 za maandalizi kabla ya mashindano hayo.

"Niliwaambia kwamba maoni yangu kuhusu wao hayabadiliki kutokana na matokeo ya wakati huo. Nilitaka waendelee kucheza kwa njia yetu, wawe jasiri, wenye nguvu, washambulie mbele na wafanye kila kitu kwa umoja," aliongeza.

Wakati wengi walikuwa wakihofia udhaifu wa safu ya ulinzi iliyoshindwa kulinda mabao mawili yaliyopatikana kupitia Harry Kane, Tuchel aliamua kuelekeza nguvu zake katika kuimarisha mchezo wa ushambuliaji.

"Ujumbe wangu ulikuwa mfupi na wa utulivu. Niliwahamasisha na kuwaambia kwamba tunawaamini na hawapaswi kuogopa chochote. Nilitaka waende kutafuta ushindi kwa kucheza kwa ujasiri zaidi," alisema.

Mabadiliko hayo yalionekana wazi kipindi cha pili ambapo England walicheza kwa kiwango cha juu dhidi ya wapinzani wao, huku mabao ya Jude Bellingham na Marcus Rashford yakihitimisha ushindi uliostahili.

"Nilikipenda sana kipindi cha pili. Nilifurahishwa na namna walivyoitikia baada ya kipindi kigumu cha kwanza," alisema Tuchel.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 52, ambaye amefundisha klabu kubwa barani Ulaya na kushinda mataji mbalimbali, alisema tatizo kubwa la timu yake katika kipindi cha kwanza lilikuwa la kisaikolojia.

"Kuongoza hakukutufanya tuwe huru zaidi. Badala yake, tulianza kufikiria jinsi ya kulinda tulichokuwa nacho. Tulipojaribu kujihami kupita kiasi, tuliadhibiwa. Lakini mwitikio wa kipindi cha pili ulikuwa wa kuvutia sana," alisema.

Tuchel alieleza kuwa kabla ya mchezo huo alikuwa ameona kikosi chake kikiwa katika hali nzuri ya kujiamini, lakini hamu kubwa ya kufanya vizuri iliwafanya baadhi ya wachezaji kuanza kufikiria kupita kiasi.

"Wakati mwingine unapohitaji kufanya jambo kwa ukamilifu mkubwa sana, unaanza kufikiria zaidi badala ya kutenda. Ndiyo maana tulikuwa tunarudisha mipira mingi nyuma na kwa kipa wetu. Hatukuthubutu kupenya kwenye nafasi zilizokuwa wazi. Ilichukua muda kurejesha kujiamini kwetu," alisema.

Licha ya ushindi huo, Tuchel amesisitiza kuwa safari bado ni ndefu, lakini ameridhishwa na hatua ya kwanza iliyopigwa na kikosi chake katika mashindano hayo makubwa.

"Imekuwa hisia kubwa sana kwangu. Tangu jana nimehisi maana ya kuwa sehemu ya Kombe la Dunia. Ni jambo la ajabu na limenifanya nijisikie hai sana ndani ya siku hizi mbili. Kwa sasa, hakuna sehemu nyingine duniani ambayo ningependa kuwa zaidi ya hapa," alisema.

Baada ya ushindi huo, England wanarejea katika kambi yao ya Kansas City huku matumaini ya mashabiki yakiongezeka kwamba safari ya kutafuta ubingwa wa dunia ambao wameusubiri kwa zaidi ya miaka 60 inaweza hatimaye kufikia mwisho wenye furaha