Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Uhamisho matata unaosubiriwa dirisha kubwa Ligi Kuu England

Muktasari:

  • Kuna mastaa kibao wanaotarajiwa kutikisa na huu hapa ni uhamisho wa nyota 22 wanaotegemewa kuhama, huku mshambuliaji wa Chelsea anaweza kuondoka. Liverpool, Chelsea, Manchester United na Real Madrid zinahusishwa zaidi na dirisha hilo kufanya mambo makubwa

LONDON, ENGLAND: UMEBAKIA mwezi mmoja tu kabla ya pilikapilika za usajili wa wachezaji kuanza kushika kasi katika ligi mbalimbali dunia, ambapo tayari majina ya mastaa kadhaa yamekuwa kwenye vichwa vya habari duniani.

Kuna mastaa kibao wanaotarajiwa kutikisa na huu hapa ni uhamisho wa nyota 22 wanaotegemewa kuhama, huku mshambuliaji wa Chelsea anaweza kuondoka. Liverpool, Chelsea, Manchester United na Real Madrid zinahusishwa zaidi na dirisha hilo kufanya mambo makubwa

Na kadri msimu unavyoingia katika hatua zake muhimu orodha ya wachezaji inaongezeka, lakini kwa sasa Daily Mail Sport imepita na mastaa hawa wakihusishwa kuondoka katika timu zao na hilo huenda likatokea likiambatana na mkwanja mzito.


JAMES TRAFFORD (MANCHESTER CITY)

Tottenham Hotspur ambao wanatarajia kumuuza Guglielmo Vicario kwenda Inter Milan, ni miongoni mwa wanaomvutiwa na kipa James Trafford, huku Aston Villa wakimsikilizia muda mrefu Emiliano Martinez na sasa anaweza kuondoka. Kutoka nje ya England kuna ofa kibao zinazomtaka Trafford, lakini kinachoelezwa ni kwamba Manchester City hawatamuuza mchezaji huyo wa kimataifa wa England kwa bei rahisi, na bei ya kati ya Pauni 35 milioni na milioni 40 inaweza kuwazuia baadhi ya wanaotaka kumsajili.

JAMES TRAFFORD (MANCHESTER CITY)

KEVIN PEDRO (ST ETIENNE)

Bournemouth na Everton wamekuwa wakifuatilia kwa karibu kuhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 katika wiki za hivi karibuni. Pedro anaweza kucheza kama beki wa kati na beki wa kulia, na amewahi kuitwa katika timu ya taifa ya Ufaransa chini ya miaka 19. Everton pia wanamfuatilia Guela Doue wa Strasbourg, lakini bei inayotakiwa inaweza kuwa kubwa kwa wachezaji wote wawili.


KARIM COULIBALY (WERDER BREMEN)

Newcastle United, Tottenham Hotspur na Chelsea wamekuwa wakimfuatilia kwa karibu Coulibaly. Mchezaji huyo wa miaka 18 wa timu ya taifa ya Ujerumani chini ya miaka 21 pia anaweza kucheza kiungo, na amekuwa na msimu mzuri akiwa Bremen akiwa amecheza mechi 22. Pia amekuwa akifuatiliwa na PSG na Real Madrid.


CASTELLO LUKEBA (RB LEIPZIG)

Beki huyo wa kati anayetumia mguu wa kushoto na anayejua kucheza akianzisha mashambulizi kutoka nyuma, Lukeba anatarajiwa kuondoka msimu huu. Mchezaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 23 anafuatiliwa na Tottenham, Chelsea, Arsenal na Manchester United huku zikipambana kufikia dau la mkataba wake wa Pauni 40 milioni.

CASTELLO LUKEBA (RB LEIPZIG)

ANDY ROBERTSON (LIVERPOOL)

Tottenham Hotspur walijaribu kumsajili Robertson kwa Pauni 4 milioni Januari, mwaka huu na watajaribu tena kama mchezaji huru mwisho wa msimu. Wengi ndani ya Liverpool wanaamini bado wanamhitaji, lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Scotland anataka kucheza mara kwa mara zaidi, na anaendelea kuzivutia klabu nyingo za England pamoja na Atletico Madrid ya Hispania.


SANDRO TONALI (NEWCASTLE UNITED)

Arsenal walifanya mawasiliano na wawakilishi Tonali huku kukiwa na uvumi juu ya Real Madrid kumtaka Declan Rice. Chelsea pia wanamfikiria Ronali, lakini Manchester United wanaonekana kuwa na nafasi nzuri zaidi kama kila kitu kitakwenda sawa. United pia wanawafuatilia Adam Wharton (Crystal Palace) na Carlos Baleba (Brighton) kwa ajili ya nafasi ya kiungo, wakitaka wachezaji wawili msimu huu wa kiangazi.


ELLIOT ANDERSON (NOTTINGHAM FOREST)

Manchester United wanamtaka Anderson kama mbadala wa Casemiro, lakini Manchester City wako katika nafasi nzuri zaidi kama wataafikiana na Forest ada ya uhamisho. City pia wanataka kuongeza mkataba mpya kwa Rodri licha ya Real Madrid kumtaka, ili kuimarisha safu ya kiungo.


HARRY WILSON (FULHAM)

Harry Wison ni mchezaji huru msimu wa kiangazi na mmoja wa wachezaji wanaofanya vizuri Ligi Kuu England. Everton walijaribu kumsajili Januari, mwaka huu lakini Fulham walimzuia, huku Aston Villa wakishinikiza kumsajili pia. Tottenham Hotspur, Leeds United na klabu nyingine pia zinamfuatilia.

HARRY WILSON (FULHAM)

SAID EL MALA (COLOGNE)

Brighton wamekuwa wakiangalia uwezekano wa kumsajili El Mala pamoja na kaka yake, Malek, ambaye ni mshambuliaji mwenye urefu wa futi 6 na inchi 4, akiwa na umri wa miaka 21. Said ana miaka 19 na ni mmoja wa mawinga wanaovutia zaidi Bundesliga, lakini Cologne wanataka kati ya Pauni 35 milioni hadi milioni 40 ili kumuachia.

Chelsea pia wameonyesha nia na wamezungumza na mama yake, Sabrina, huku Brentford na Fulham pia wakifanya mawasiliano.


YAN DIOMANDE (RB LEIPZIG)

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 anathaminishwa kwa karibu Pauni 87 milioni. Liverpool wamekuwa wakimtamani muda mrefu, lakini bei yake ni kubwa na bado hawana uhakika wa kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Manchester United, Arsenal na Tottenham Hotspur pia wameulizia uwezekano wa kumpata katika timu yake ya RB Leipzig, huku PSG na Bayern Munich wakifuatilia kwa karibu.


LIAM DELAP (CHELSEA)

Chelsea wanataka mabao zaidi na wanatafuta mshambuliaji mpya wa kati. Mbali na Emmanuel Emegha wa Strasbourg, pia walimfikiria Joaquin Panichelli kabla ya kupata jeraha la goti msimu uliopita kisha wakadondokea kwa Delap. Hata hivyo msimu huu mambo si mambo kwake. Kwa sasa Newcastle United na Everton wanamfuatilia Delap wakiamini angefaidika na muda wa kucheza mara kwa mara kama alivyofanya Ipswich, lakini mambo yamemwendea kombo.

LIAM DELAP (CHELSEA)

TIMU YA PILI (SECOND XI) ROBIN ROEFS (SUNDERLAND)

Mmoja wa usajili bora wa msimu, Roefs ameivutia klabu nyingi za Ligi Kuu England na nje ya England. Sunderland wanataka kumbakiza, lakini wanatarajia ofa kwa mchezaji huyo mwenye miaka 23 aliyesajiliwa kwa Pauni 8.5 milioni kutoka NEC Nijmegen, ambao wana kipengele cha kupata asilimia ya mauzo yake.


JHON LUCUMI (BOLOGNA)

Sunderland walikataliwa ofa zao msimu uliopita na bado wanamfuatilia, huku Bournemouth pia wakiwa miongoni mwa wanaoulizia. Hata hivyo, klabu nyingine za Ligi Kuu England zinatuma maskauti kumtazama beki huyo wa kati wa Colombia mwenye miaka 27.


VICTOR VALDEPENAS (REAL MADRID)

Arsenal wanampenda nyota huyo mwenye umri wa miaka 19 anayeweza kucheza beki wa kushoto na kati. Pia wamekuwa wakimfuatilia Jacobo Ramon aliyekuwa akademi ya Real Madrid na anayefanya vizuri chini ya Cesc Fabregas huko Como, na pia yupo kwenye orodha ya wachezaji wanaotakiwa na Chelsea majira ya kiangazi.


NECO WILLIAMS (NOTTINGHAM FOREST)

Kama ilivyo kwa wachezaji wengi wa Nottingham Forest, Williams anavutia klabu nyingi kadri msimu unavyokaribia kumalizika. Iwapo Forest watashuka Ligi Kuu England atakuwa rahisi zaidi kuondoka, ingawa mmiliki wa timu hiyo, Evangelos Marinakis bado anaweza kuzuia mauzo.


VALENTIN BARCO (STRASBOURG)

Chelsea wanataka kumsajili beki huyo wa zamani wa Brighton ambaye pia anaweza kucheza kiungo na winga.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 pia ni sehemu ya timu ya taifa ya Argentina. Strasbourg walilipa Pauni 8.5 milioni ili kumchukua kutoka Brighton ambao bado wana kipengele cha asilimia ya mauzo.


ADAM WHARTON (CRYSTAL PALACE)

Wharton amevutia klabu zote kubwa Ulaya na anathaminishwa karibu Pauni 65 milioni. Maswali kwa baadhi ya klabu kama Liverpool ni kama ana uwezo wa kukimbia zaidi katika timu zinazomiliki mpira, lakini Real Madrid, Chelsea, Manchester United na Tottenham Hotspur zote zinaamini ana uwezo mkubwa wa kupiga pasi sahihi.


KEES SMIT (AZ ALKMAAR)

Newcastle United imekuwa ikimfuatilia kwa muda mrefu Kees Smit, lakini inakabiliwa na ushindani mzito. Liverpool, Manchester United, Chelsea, Arsenal, PSG, Barcelona na Real Madrid pia zinamwangalia kwa jicho la karibu. Nyota huyo anachukuliwa kuwa 'Kevin De Bruyne' ajaye.


YANKUBA MINTEH (BRIGHTON)

Yankuba amekuwa na msimu wenye mchanganyiko wa ubora na ubovu, lakini uwezo wake wa kuamua mchezo kwa vipindi fulani ni mkubwa. Bado ni kijana mwenye umri wa miaka 21 akiwa na kasi kubwa, lakini anahitaji kuboresha ufungaji wake. Alikuwa chini ya Arne Slot huko Feyenoord na anaweza kuingia kwenye mipango ya Liverpool endapo Slot ataendelea kubaki. Arsenal na Tottenham Hitspur pia wanavutiwa naye.

YANKUBA MINTEH (BRIGHTON)

JARROD BOWEN (WEST HAM)

Iwapo West Ham United watashuka daraja, Bowen atakuwa miongoni mwa wachezaji wanaotafutwa sana ndani na nje ya England. Amekuwa tegemeo la klabu hiyo na anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha England katika Kombe la Dunia 2026. West Ham wanataka angalau Pauni 50 mili kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 aliyesaliwa na miaka minne kwenye mkataba wake.


JACK GREALISH (MANCHESTER CITY)

Anaendelea na mazoezi ya majeraha akiwa Everton badala ya Manchester City, jambo linaloutesa mtazamo wake kuhusu nafasi yake chini ya Pep Guardiola kule Man City na timu ya taifa ya England kwa Kombe la Dunia 2026. Kwa sasa anacheza kwa mkopo Everton. Everton wameshasema tangu Oktoba, mwaka jana kwamba wanataka kumsajili kwa Pauni 30 milioni, lakini bado kuna mazungumzo magumu kufikia makubaliano.


CHRISTIAN KOFANE (BAYER LEVERKUSEN)

Nyota huyo analinganishwa na mkongwe wa kimataifa wa Cameroon na Barcelona, Samuel Eto’o, lakini bado anahitaji kuboresha uwezo wake wa kufunga. Kofane anachukuliwa kuwa mmoja wa washambuliaji chipukizi bora Bundesliga, na klabu kama Arsenal, Chelsea, Real Madrid na Everton zimekuwa zikimfuatilia.