Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Uefa Super Cup... Kuna mtu atapigika!

SUPER Pict

Muktasari:

  • Kwa kifupi tu, kipute hicho kitahusisha miamba miwili, Paris St-Germain ambao ni mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na Tottenham Hotspur walionyakua Europa League msimu uliopita. Patachimbika.

UDINE, ITALIA: MAMBO ni moto. Kipute cha Uefa Super Cup kinapiga Jumatano usiku na mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya wataonyeshana kazi na washindi wa Europa League huko Udine, Italia.

Kwa kifupi tu, kipute hicho kitahusisha miamba miwili, Paris St-Germain ambao ni mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na Tottenham Hotspur walionyakua Europa League msimu uliopita. Patachimbika.

Mechi hiyo itafanyika kwenye uwanja unaoingiza watazamaji 25,000 tu, Stadio Friuli, ambao unatumiwa na timu ya Udinese kwenye mechi za Serie A.

Huo utakuwa uwanja wa 13 kutumika kwenye mechi hiyo inayofanyika kila mwaka tangu ilipohamishwa kutoka Monaco 2012 na kutumia viwanja tofauti.

Timu yoyote itakayochukua ubingwa kwa usiku huo, basi itakuwa ni mara ya kwanza kwao.

PSG imekata tiketi ya kucheza mechi hiyo baada ya kuichapa Inter Milan mabao 5-0 katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita, wakati Spurs tiketi yake imepata baada ya kushinda dhidi ya Manchester United 1-0 kwenye fainali ya Europa League miezi mitatu iliyopita.

Real Madrid ndio mabingwa watetezi wa Uefa Super Cup kwa sasa baada ya kuwachapa Atalanta 2-0 mwaka jana, shukrani kwa mabao ya Federico Valverde na Kylian Mbappe.


Uefa Super Cup ni nini?

Taji hilo lilikuwa pendekezo la mwandishi mmoja wa Kidachi, Anton Witkamp, aliyetaka ichezwe mechi ili ipatikane timu moja ambayo itakuwa bingwa wa Ulaya. Ajax iliichapa Rangers kwenye mechi mbili, wakati michuano hiyo ilipoanza mwaka 1972, lakini wazo hilo lilifanywa kuwa rasmi na Uefa 1973.

Super Cup mwanzoni ilikuwa ikichezwa kwa kuwakutanisha washindi wa Kombe la Ulaya wakati huo na mabingwa wa Kombe la Washindi.

Na baada ya Kombe la Washindi kufutwa na Uefa mwaka 1999, mechi hiyo sasa ya Uefa Super Cup imekuwa ikifanyika mara moja kwa mwaka kwa kukutanisha mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya washindi wa Europa League. Licha ya kuongezeka kwa mashindano ya Conference League kwaka 2021, washindi wake hawachezi kwenye Super Cup.

Real Madrid imebeba Uefa Super Cup mara sita na kuwa timu iliyobeba taji hilo mara nyingi zaidi kihistoria.

Uefa inachaguaje uwanja wa Super Cup?

Uefa Super Cup ilikuwa ikifanyika Monaco kuanzia 1998 hadi 2012, lakini baada ya hapo imechezwa kwenye viwanja 13 tofauti.

Sasa uwanja wa mechi unapatikana kwa mashirikisho ya soka ya nchi kupambana kuomba kuandaa mechi hiyo kabla ya kamati ya utendaji ya Uefa kufanya uamuzi wa mwisho wa kuteua uwanja wa mechi kwa mwaka husika.

Bingwa wa Uefa Super Cup itapewa zawadi ya pesa, Euro 5 milioni, wakati timu itakayokuwa imepoteza mechi itaweka kibindoni, Euro 4 milioni.

PSG: Chevalier; Hakimi, Marquinhos, Pacho, Nuno Mendes; Zaire-Emery, Vitinha, Fabian Ruiz; Doue, Dembele, Kvaratskhelia

Spurs: Vicario; Pedro Porro, Romero, Van de Ven, Spence; Bentancur, Palhinha, Sarr; Johnson, Richarlison, Kudus.