Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Uefa kususia Kombe la Dunia

Muktasari:

  • Kwa wiki kadhaa sasa, Trump amekuwa akisisitiza Marekani lazima iipate Greenland ambayo ni kisiwa kikubwa zaidi duniani akidai ni kwa sababu za usalama wa taifa lake.

NYON, SWITZERLAND: VIONGOZI wa soka Ulaya wamefanya mazungumzo ya awali kuhusu hatua wanazoweza kuchukua ili kujibu kile kinachofanywa na Rais wa Marekani, Donald Trump kutaka kuichukua Greenland mikononi mwa Denmark na inaelezwa wanaweza kususia mashindano ya Kombe la Dunia yatayofanyika baadae mwaka huu huko Marekani, Canada na Mexico.

Kwa wiki kadhaa sasa, Trump amekuwa akisisitiza Marekani lazima iipate Greenland ambayo ni kisiwa kikubwa zaidi duniani akidai ni kwa sababu za usalama wa taifa lake.

Trump ametishia pia kutoza ushuru mkubwa kwa nchi ambazo hazitaunga mkono mpango wake.

Hali hiyo inadaiwa kusababisha Uefa kufikiria kususia Kombe la Dunia na nchi zote za Ulaya hazitokwenda katika mashindano hayo.

Ripoti kutoka gazeti la The Guardian inaeleza takribani viongozi 20 wa vyama vya soka Ulaya walifanya mazungumzo kuhusu namna ambavyo wanaweza kuchukua hatua, walipokutana katika hafla ya hivi karibuni jijini Budapest ya kuadhimisha miaka 125 ya Shirikisho la Soka la Hungary.

Kundi kubwa la viongozi wa vyama vya soka vya Ulaya walisema wasusie michuano hiyo ikiwa tu Marekani itapeleka jeshi lake katika visiwa hivyo na sio tu kususia Kombe la Dunia, pia wanaweza kuchukua hatua nyingine.

“Vyama vingi vya soka vinataka kufuata misimamo ya serikali zao kuhusu matukio yanayohusu Greenland. Kuna imani ikiwa moja ya vyama vikubwa vya soka Ulaya vingetangaza kutoshiriki na vingine pia vingefuata."

Mwanasiasa wa Ujerumani, Jurgen Hardt, hivi karibuni alipendekeza hatua ya kususia mashindano ifanywe kuwa ya mwisho lakini kwa sasa iangaliwe namna nzuri ya kufanya majadiliano.