Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Trent Alexander-Arnold alimwaga

Muktasari:

  • Beki huyo wa kulia mwenye uwezo wa kucheza kiungo ya kati mkataba wake wa sasa huko Anfield utafika tamati mwishoni mwa msimu huu.

LIVERPOOL, ENGLAND: TRENT Alexander-Arnold amewaambia mabosi wa Liverpool kwamba hatasaini mkataba mpya na anachotaka ni kwenda kujiunga na Real Madrid.

Beki huyo wa kulia mwenye uwezo wa kucheza kiungo ya kati mkataba wake wa sasa huko Anfield utafika tamati mwishoni mwa msimu huu.

Lakini, pamoja na kwamba amekuwa na mapenzi makubwa na klabu yake, Alexander-Arnold anataka kwenda kukabiliana na changamoto mpya kwenye dirisha lijalo la majira ya kiangazi na mpango wake ni kwenda kukipiga Santiago Bernabeu. Taarifa za kutoka Hispania zinadai kwamba, Trent, 26, amewaambia mabosi wa Anfield dhamira yake ya kwenda kukipiga Real Madrid kwa uhamisho wa bure dirisha la majira ya kiangazi mwakani.

Alexander-Arnold ni mmoja wa mastaa watatu wa maana kabisa wa Liverpool, sambamba na Mohamed Salah na Virgil van Dijk ambao mikataba yao itafika tamati mwishoni mwa msimu huu.

Kinachoelezwa ni kwamba Los Blancos, ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, wamepanga kuanza mazungumzo na mchezaji huyo wakati dirisha la Januari litakapofunguliwa.

Hata hivyo, Liverpool wao kwao ni heri wamwaache beki huyo aondoke bure mwisho wa msimu kuliko kumfungulia mlango wa kutokea kwenye usajili wa dirisha la mwezi ujao. Mpango wao wanataka kubaki na mchezaji huyo ili kuwasaidia kushinda taji la Ligi Kuu England msimu huu kabla ya kumruhusu aondoke.

Trent akifanikiwa kutua Real Madrid atakwenda kucheza na swahiba wake na mchezaji mwenzake wa timu ya taifa ya England, Jude Bellingham.

Beki wa zamani wa Liverpool, Jamie Callagher alisema kuhusu ishu ya Trent akisema: “Kama akibaki, atakumbukwa kama mmoja wa wachezaji mahiri waliowahi kuchezea Liverpool sambamba na Steven Gerrard. Kama ataondoka, hatakumbukwa kwa hilo.”