Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Trent aanza kwa mkosi Madrid

Muktasari:

  • Trent, 26, alianzishwa mara mbili katika mechi nne za kwanza za La Liga akiwa na Real Madrid, alionekana kupata maumivu ya misuli ya paja katika mchezo huo wa Jumanne dhidi ya Marseille uwanjani Bernabeu. Kutokana na hilo, nafasi yake ya kucheza dhidi ya timu yake ya zamani, Liverpool kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa muda usiozidi miezi miwili ipo kwenye hatari kubwa kutotimia.

MADRID, HISPANIA: BEKI Trent Alexander-Arnold ameanza vibaya maisha kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Real Madrid baada ya kuumia dakika ya tano na kushindwa kuendelea na mchezo.

Trent, 26, alianzishwa mara mbili katika mechi nne za kwanza za La Liga akiwa na Real Madrid, alionekana kupata maumivu ya misuli ya paja katika mchezo huo wa Jumanne dhidi ya Marseille uwanjani Bernabeu. Kutokana na hilo, nafasi yake ya kucheza dhidi ya timu yake ya zamani, Liverpool kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa muda usiozidi miezi miwili ipo kwenye hatari kubwa kutotimia.

Alexander-Arnold anajiandaa kurudi Anfield kwa mara ya kwanza tangu alipoachana na timu hiyo mwishoni  mwa msimu uliopita akijiunga na Los Blancos. Mechi hiyo ya kibabe baina ya Liverpool na Real Madrid imepangwa kufanyika Novemba 4.

Timu hizo zote zinahitaji kushinda ili kuwamo kwenye nafasi nane za juu kwenye msimamo ili kufuzu hatua ya mtoano moja kwa moja bila ya kuhitaji mechi nyingine za mchujo.

Alexander-Arnold alianza kuhisi maumivu ya misuli ya paja la mguu wa kulia dakika ya pili tu ya mchezo baada ya kupiga pasi kwenye mechi dhidi ya Marseille.

Beki huyo wa kulia alilazimika kukaa chini uwanjani na kuhitaji huduma ya madaktari. Na hapo ilithibitika kwamba Alexander-Arnold alishindwa kuendelea na mchezo.  Alitolewa na kuingizwa Dani Carvajal, ambaye alianzishwa kwenye mechi ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Real Sociedad kwenye La Liga, Jumamosi iliyopita.

Na sasa Alexander-Arnold anakimbizana na muda kuwa fiti kabla ya kipute cha Anfield, mechi ambayo inatarajiwa kuwa na umuhimu mkubwa kwa mchezaji huyo wakati atakaporejea kuikabili timu yake ya zamani  Liverpool.