Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tottenham weka bei kubwa Romero, Dola 50–70 Milioni

Muktasari:

  • Akizungumza na Cadena 3, Victor Romero ambaye ni baba wa beki huyo alithibitisha kiwango cha kifungu cha kuachiwa kwa nahodha huyo wa Tottenham Hotspur kwamba ni kati ya Dola 50 milioni hadi 70 milioni, hivyo kama kuna timu inafikiria kumfuata ikiwa na pungufu ya mzigo huo haitaambulia kitu.

BUENOS AIRES, ARGENTINA: Iwapo klabu pinzani zinamtaka Cristian Romero, hawatapatikani kwa bei rahisi, kwa mujibu wa baba yake aliyezungumzia hatima ya mwanaye katika kikosi cha Tottenham Hotspur akisema hata kama itashuka, lakini nahodha huyo hatakamatika kirahisi sokoni.

Akizungumza na Cadena 3, Victor Romero ambaye ni baba wa beki huyo alithibitisha kiwango cha kifungu cha kuachiwa kwa nahodha huyo wa Tottenham Hotspur kwamba ni kati ya Dola 50 milioni hadi 70 milioni, hivyo kama kuna timu inafikiria kumfuata ikiwa na pungufu ya mzigo huo haitaambulia kitu.

“Bado ana miaka miwili kwenye mkataba wake na Tottenham na ana kifungu cha kuachiliwa chenye thamani kubwa sana. Klabu hiyo ya England haitamwachia aondoke bure; ni kati ya Dola milioni 50–70. Kwa mtazamo wangu, watataka kurejesha kile walichowekeza,” alisema Victor.

Agosti 2021 Spurs walimsajili Romero kutoka Atalanta ya Italia kwa Pauni 43 milioni kikiwa ni kiwango cha ada kilichomfanya kuwa mchezaji wa pili ghali zaidi katika historia ya klabu hiyo wakati huo.

Tangu hapo, Romero amecheza mechi zaidi ya 150 katika mashindano yote na alikuwa na mchango mkubwa kumaliza ukame wa miaka 17 wa klabu hiyo kutwaa taji msimu uliopita katika Europa League.

Licha ya hadhi yake klabuni, Romero amekuwa akihusishwa mara kwa mara na uhamisho kwenda Atletico Madrid ya Hispania, ambapo iliripotiwa Mei, mwaka jana kuwa mshindi huyo wa Kombe la Dunia yupo tayari kuhamia katika kikosi hicho cha kocha Diego Simeone.

Hata hivyo, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alionekana kuzima tetesi hizo kwa kusaini mkataba mpya wa miaka minne Agosti, mwaka jana, unaomfunga Tottenham hadi 2029.

Miongoni mwa klabu zinazotajwa kumtaka pia ni ile ya utotoni, Atletico Belgrano. Romero alianzia soka lake hapo na alicheza mechi 19 kikosi cha kwanza kabla ya kuhamia Genoa ya Italia, Julai 2018.

Hata hivyo, kama baba yake alivyosema, “kila kitu kinawezekana” katika soka na alipoulizwa kuhusu tetesi hizo, Victor alisema: “Hii ni habari kubwa inayozidi kukua. Natumaini ni kweli. Kama shabiki wa Belgrano na baba ningetaka nini zaidi? Lakini sina uhakika wowote.

Klabu hiyo ya kaskazini mwa London ipo nafasi ya 17, pointi moja tu juu ya eneo la kushuka daraja huku zikiwa zimebaki mechi saba. Spurs pia itaingia katika hatua ya mwisho ya msimu ikiwa na kocha wa tatu baada ya Roberto De Zerbi kupewa mkataba wa miaka mitano usiojumuisha kipengele cha kushuka daraja na mechi yake ya kwanza  itakuwa ugenini dhidi ya Sunderland Aprili 12.