Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Timu kuongezwa Kombe la Dunia la Klabu, EPL ikinufaika

FIFA Pict

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali, ushirikiano huo unatarajiwa kufungua milango kwa klabu nyingi zaidi kutoka Ligi Kuu England kushiriki mashindano hayo, jambo ambalo litakuwa pigo kwa timu zilizokuwa zikikosa nafasi kutokana na kanuni zilizokuwapo awali.

ZURICH, USWISI: SHIRIKISHO la Soka Duniani (FIFA) linatarajiwa kufanya mabadiliko makubwa zaidi katika historia ya Kombe la Dunia la Klabu baada ya kuanza mchakato wa kupanua mashindano hayo kutoka timu 32 hadi 48 kuanzia mwaka 2029.

Hatua hiyo inakuja baada ya FIFA kufikia makubaliano ya kuunda ubia mpya na kundi la Klabu za Ulaya (EFC), linalowakilisha zaidi ya klabu 700 barani humo na linaloongozwa na Rais wa Paris Saint-Germain, Nasser Al-Khelaifi.

Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali, ushirikiano huo unatarajiwa kufungua milango kwa klabu nyingi zaidi kutoka Ligi Kuu England kushiriki mashindano hayo, jambo ambalo litakuwa pigo kwa timu zilizokuwa zikikosa nafasi kutokana na kanuni zilizokuwapo awali.

FIF 01

Katika toleo la kwanza la mashindano yaliyopanuliwa na kushirikisha timu 32, baadhi ya mabingwa wa ligi kubwa za Ulaya walishindwa kushiriki kutokana na FIFA kuweka kikomo cha timu mbili kutoka kila nchi pamoja na kuzingatia washindi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na viwango vya ubora vya UEFA.

Kutokana na mfumo huo, klabu kadhaa kubwa zilikosa nafasi ya kushiriki licha ya ubora wao, hali iliyozua mjadala mkubwa ndani ya soka la Ulaya.

Sasa, EFC inataka sheria ya kikomo cha timu mbili kutoka nchi moja kuondolewa ili kutoa nafasi kwa timu nyingi zaidi kutoka ligi zenye ushindani mkubwa, hususan England.

FIF 02

Iwapo pendekezo hilo litapitishwa, klabu kama Arsenal, Liverpool na Manchester City zinaweza kunufaika na kupata nafasi ya kushiriki mashindano hayo kutokana na nafasi zao nzuri katika viwango vya UEFA.

FIFA inaamini kuongeza idadi ya klabu za Ulaya kutasaidia kuongeza thamani ya kibiashara ya mashindano hayo, hususan katika mikataba ya haki za matangazo na udhamini.

Sababu kubwa ya kuongezwa kwa timu hizo ni mafanikio ya kifedha yaliyopatikana katika toleo la kwanza la mashindano hayo. Chelsea, ambao walitwaa ubingwa wa mashindano hayo, waliripotiwa kuingiza takribani Pauni 84 milioni kutokana na ushindi huo.

Mafanikio hayo yamezifanya klabu nyingi kubwa za Ulaya kuishinikiza FIFA kuongeza idadi ya washiriki ili kuongeza nafasi zao za kushiriki na kunufaika kifedha.

Hata hivyo, bado kuna changamoto zinazopaswa kutatuliwa kabla ya kuanza kwa mfumo mpya. Miongoni mwa masuala yanayosubiri ufumbuzi ni namna ya kugawanywa kwa kiasi cha Pauni 185 milioni kilichotengwa kama fedha za mshikamano kwa klabu mbalimbali duniani.

FIF 03

Pia, mashirikisho sita ya mabara bado hayajafikia mwafaka kuhusu mfumo wa ugawaji wa fedha hizo.

Ushirikiano mpya kati ya FIFA na EFC unaashiria kuimarika kwa mahusiano kati ya FIFA na klabu kubwa za Ulaya, baada ya awali pande hizo kuwa na tofauti wakati wa maandalizi ya toleo la kwanza la Kombe la Dunia la Klabu lililofanyika Marekani.

Mara baada ya masuala ya kifedha kukamilika, mjadala mkubwa utahamia katika maandalizi ya mashindano ya mwaka 2029, ambayo yanaweza kushirikisha jumla ya timu 48 kwa mara ya kwanza katika historia ya mashindano hayo.