Tiger Woods avunja ukimya baada ya ajali na kukamatwa
Muktasari:
- Woods mwenye miaka 50 aliachiwa kwa dhamana baada ya ajali hiyo kutokea Florida. Picha za ajali zilionyesha gari lake aina ya Land Rover lililokuwa limepinduka kando ya barabara eneo la Jupiter Island, Florida.
LAS VEGAS, MAREKANI: MCHEZAJI mashuhuri wa gofu, Tiger Woods amevunja ukimya na kuwaambia mashabiki wake kuwa anapambana kuwa sawa kiafya baada ya ajali ya gari, ambayo ilimsababisha kukamatwa kwa tuhuma za kukiuka sheria za kuendesha akiwa amelewa au kutumia dawa za kulevya (DUI).
Woods mwenye miaka 50 aliachiwa kwa dhamana baada ya ajali hiyo kutokea Florida. Picha za ajali zilionyesha gari lake aina ya Land Rover lililokuwa limepinduka kando ya barabara eneo la Jupiter Island, Florida.
Polisi ilimkuta Woods na makosa matatu tofauti ikiwemo kuendesha akiwa na pombe au dawa za kulevya, uharibifu wa mali na kushindwa kufanya mtihani wa kisheria wa pombe hivyo aliwekwa rumande kwa saa nane.
Akiongea kwa mara ya kwanza baada ya tukio hilo, Woods aliwashukuru mashabiki wake kwa msaada na kusema kuwa anapumzika kwa kipindi fulani.
Alisema: “Ninaelewa uzito wa hali niliyomo. Ninaachana kwa muda ili kupata matibabu na kuzingatia afya yangu. Hii ni muhimu ili kuweka ustawi wangu, niimejitolea kutumia muda huu kurudi katika hali nzuri zaidi, yenye nguvu na umakini. Nashukuru kuelewa kwenu na msaada na ninaomba faragha kwa familia yangu, wapendwa wangu na mimi mwenyewe kwa wakati huu.” Polisi walisema Woods alionyesha dalili za kushindwa kudhibi mwendo kwenye usafiri wake, lakini baadaye wakasema walikuwa “hawana shaka kuwa pombe ilihusika” baada ya kumpima kwenye kipimo cha pumzi.