Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Terry aibua upya suala la Abramovich

TERRY Pict

Muktasari:

  • Bilionea huyo mfanyabiashara wa Russia aliinunua Chelsea mwaka 2003 na aliifanya timu hiyo kupata mafanikio makubwa ndani ya uwanja kutokana na uwekezaji wake.

LONDON, ENGLAND: ALIYEKUWA beki wa kati wa Chelsea, John Terry ameamua kuishambulia serikali ya Uingereza baada ya kumlazimisha bilionea Roman Abramovich kuipiga bei The Blues baada ya Russia kuivamia kijeshi Ukraine miaka mitatu na nusu iliyopita.

Bilionea huyo mfanyabiashara wa Russia aliinunua Chelsea mwaka 2003 na aliifanya timu hiyo kupata mafanikio makubwa ndani ya uwanja kutokana na uwekezaji wake.

Waziri Mkuu wa Uingereza kwa wakati huo, Boris Johnson, alimfungia biashara zake Abramovich, Machi 2022, jambo lililomfanya tajiri huyo  Russia kulazimika kuipiga bei Chelsea kwa tajiri wa Marekani na washirika wake, Todd Boehly.

Zuio hilo la tajiri Abramovich limeendelea hata sasa wakati wa serikali ya Sir Keir Starmer, huku Pauni 2.5 bilioni zilizopatikana kwenye mauzo ya klabu hiyo bado zimeshikiliwa na benki za Uingereza.

Beki Terry sasa ameonyesha hasira zake juu ya jambo hilo, aliposema: "Nadhani ni mtu mwenye moyo safi niliyewahi kukutana naye kwenye maisha yangu. Nadhani ni kitu kinachoshangaza sana kilichomtokea, nimehuzunika sana. Nadhani serikali ya Uingereza tunapaswa kuwa na aibu kwa kile tulichomfanyia. Ona kile alichokifanya kwenye kipindi cha kujifungia ndani wakati wa janga la uviko 19 kwenye idara ya afya. Alifungua milango ya uwanja wa Stamford Bridge kwa manesi wote na kuwapa watu makazi katika kipindi kigumu."

Terry alifunguka zaidi juu ya uhusiano wake na Abramovich na kusema: "Nadhani kila mtu ana uhusiano mzuri na yeye. Ninachoweza kusema ni mmoja wa watu safi niliowahi kukutana naye."