Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ten Hag kupewa mchongo Feyenoord

Muktasari:

  • Ten Hag, 55, alifutwa kazi Manchester United, Oktoba mwaka jana baada ya timu hiyo kuanza msimu vibaya kwa matokeo ya hovyo.

ROTTERDAM, UHOLANZI: ERIK ten Hag muda wowote simu yake inaweza kuita kwa ajili ya kupewa mchongo wa kwenda kuinoa Feyenoord ya huko kwao Uholanzi, imeelezwa.

Ten Hag, 55, alifutwa kazi Manchester United, Oktoba mwaka jana baada ya timu hiyo kuanza msimu vibaya kwa matokeo ya hovyo.

Lakini, klabu ya Feyenoord yenye maskani yake Rotterdam inamtaka Ten Hag kwenda kuwa kocha wao mpya baada ya kumfuta kazi Brian Priske, Jumatatu.

Rene Hake, aliyekuwa msaidizi wa Ten Hag huko Old Trafford, naye anapigiwa hesabu za kwenda kuwa kocha msaidizi katika klabu hiyo ya De Kuip.

Ten Hag alishinda Kombe la FA na Kombe la Ligi kwa misimu yake miwili aliyokuwa kwenye kikosi cha Man United.

Huko nyuma alikuwa kwenye kikosi cha Ajax ambao ni mahasimu wa Feyenoord kwa kipindi cha misimu minne na kuwapa mataji matatu ya Eredivisie na mataji mawili ya Kombe la Uholanzi. Ten Hag aliwahi kuzinoa pia klabu za Utrecht na Go Ahead Eagles, ambazo pia ni za Uholanzi.

Feyenoord imechukua kocha wao wa timu ya Under-21, Pascal Bosschaart kukinoa kikosi cha wakubwa kwa muda.

Mkurugenzi, Dennis te Kloese alisema: "Tumefurahi Pascal amekuwa na utayari wa kuchukua mikoba kwa muda. Nimezungumza na wachezaji na makocha na kila mtu na wameonyesha kwamba wapo tayari kwa mapambano."

Feyenoord inashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Eredivisie kwa sasa, pointi 12 nyuma ya vinara Ajax. Hata hivyo, bado ipo kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu, ambapo usiku wa jana Jumatano ilitarajia kucheza mechi yake ya kwanza ya mchujo dhidi ya AC Milan huko Uholanzi.